Tafuta

Vatican News
2020.05.27 - Charles de Foucauld (1858-1916) mmisionari nchini Algeria atatangazwa kuwa Mtakatifu 2020.05.27 - Charles de Foucauld (1858-1916) mmisionari nchini Algeria atatangazwa kuwa Mtakatifu 

Papa Francisko aridhia kutangazwa kwa watakatifu wapya wa Kanisa!

Padre Charles de Foucauld atatangazwa Mtakatifu.Michael McGinvey,Mwanzilishi wa Shirika Kijeshi la Colombus atatangazwa mwenye heri.Hata Pauline Jaricot,Mwanzilishi wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa,PMS.Ni orodha ya watu muhimu watakatifu wapya na wenye heri walioridhiwa na Papa Francisko tarehe 26 Mei 2020 baada ya Mkutano na Kardinali Angelo Becciu,Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza wenye heri.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 26 Mei 2020, Papa Francisko alikutana na Kardinali Angelo Becciu, Rais wa Baraza la kipapa la kuwatangaza wenye heri na Watakatifu. Katika mkutano huo  Papa alilidhia Baraza hilo kuwatangaza wenye heri na watakatifu wafuatao: mujiza uliyotokea kwa maombezi ya Mwenye heri Cesare de Bus, Padre na mwanzilishi wa Shirika la Mapadre wa Mafundisho ya Kikristo (Dottrinari); Alizaliwa tarehe 3 Februari 1544 huko Cavaillon (Ufaransa) na kifo chake huko Avignone (Ufaransa) tarehe 15 Aprili 1607; Miujiza kwa ajili ya maombezi ya Mwenye heri  Charles de Foucauld (aitwaye Charles wa Yesu), Padre wa kijimbo; alizaliwa Strasburg (Ufaransa );tarehe 15 Septemba 1858 na kifo chake huko Tamanrasset  nchini (Algeria) tarehe 1 Desemba 1916.

Hali kadhalika miujiza kwa maombezi ya Beata Maria Domenica Mantovani, Mwanzishi Msaidizi na Mkuu wa kwanza wa Shirika la Watawa wadogo wa Familia Takatifu; Alizaliwa tarehe 17 Novemba 1862 huko Castelletto ya Brenzone (Italia) na kifo chake tarehe 2 Februari  1934; Miujiza kwa maombezi ya Mtumishi wa Mungu Michele McGivney, Padre wa jimbo na Mwanzilishi wa Shirika la Kijeshi la Columbus,(The Knights of Columbus); Alizaliwa tarehe 12 Agosti 1852 huko Waterbury (Marekani) na kifo chake huko Thomaston (Marekani) tarehe  14 Agosti 1890.

Vile vile Papa Francisko ameitambua miujiza kwa maombezi wa Mtumishi wa Mungu Paolina Maria Jaricot, Mwanzilishi wa Mashirika ya Kimisionari ya kipapa na rosari iliyo hai; Alizaliwa tarehe 22 Julai  1799 huko  Lione (Ufaransa ) na kifo chake tarehe 9 Januari 1862; Kifodini cha Mtumishi wa Mungu Simeone Cardon na wenzake watawa wa 5 wa Shirika la Cistercense la Casamari; waliouwawa kwa sababu ya chuki ya imani yako kati ya tarehe 13 na  16 Mei 1799.

Mfiadini, Mtumishi wa Mungu Cosma Spessotto,  Padre wa Shirika la Ndugu Wadogo wafransiskani; Alizaliwa tarehe 26 Januari 1923 huko Mansué (Italia) na kuuwawa huko San Juan Nonualco (El Salvador), kwa sababu ya chuki ya imani yake kunako tarehe 14 Juni 1980; na hatimaye, fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Melchiorre Maria de Marion Brésillac, Askofu wa  Prusa, na Mwanzilishi wa Chama cha kimisionari cha Afrika; Alizaliwa tarehe 2 Desemba 1813 huko Castelnaudary (Ufaransa) na kifo chake huko Freetown(Sierra Leone) tarehe  25 Juni 1859.

27 May 2020, 14:30