Tafuta

Vatican News
Vatican Vatican  

Papa Francisko amemteua Makamu Camerlengo na Balozi wa Iraq

Askofu Mkuu Ilson de Jesus Montanari ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Makamu Camerlengo wa Kanisa Takatifu la Roma.Pia Papa amemteua Balozi wa Kitume nchini Iraq Monsinyo Mitja Leskovar.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mei Mosi 2020 Papa Francisko amemteua Askofu Mkuu Ilson de Jesus Montanari wa Capocilla ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu kuwa makamu mkuu “Camerlengo” wa Kanisa Katoliki la Roma, ambaye atakuwa atasaidiana na  Kardinali Kevin Joseph Farrell, Rais wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha ambaye aliteuliwa kunako tarehe 14 Februari 2019 ili kuchukua madaraka hayo. Hii  ina maana ya kuchukua majukumu kama Mhazini wa Kanisa” aliye na  dhamana ya kuratibu masuala yote ya fedha na mali ya Kanisa kwa muda. Dhamana hii inatekelezwa hasa zaidi wakati ambapo kiti cha Ukulu wa Mtakatifu Petro kinaweza kubaki wazi, kufuatia na kifo cha  kharifa wake.

Aidha katika siku hii ya Mei Mosi, Papa Francisko amemteua Balozi wa Kitume nchini Iraq Monsinyo Mitja Leskovar, mshauri wa Ubalozi na kupewa moja kwa moja hadhi ya uaskofu mkuu wa makao ya Benevento. Alizaliwa kunako tarehe 3 Januari 1970 huko  Kranj, nchini  Slovenia, alipewa daraja la upadre kunako tarehe 29 Juni 1995. Aliingia katika huduma ya kidiplomasia Mjini Vatican kuanzia tarehe 1 Julai 2001, na kutoa huduma yake katika uwakilisho wa kipapa nchini Bangladesh, katika kitengo cha Katibu Mkuu wa kwa ajili ya uhusiano na ushrikiano wa kimataifa na kuwakilisha katika balozi za kitume nchini Ujerumani na India

Mambo mengine mapya hata katika Baraza la Maaskofu. Katika Mkutano kuhusu masuala ya ndani uliofanyika tarehe 14 Aprili 2020, Papa aliamua kujumuika katika Agizo la Maaskofu, kwa kumpatia Kardinali Luis Antonio G. Tagle, Kanisa la Mtakatifu Felice wa Cantalice huko Centocelle, ambaye ni Rais wa Baraza la Kipapa la  Uinjilishaji wa Wat una kwa maana hiyo maa uamuzi wake umeanza rasmi Mei Mosi. Na zaidi Papa Francisko amemwinua Kardinali Beniamino Stella, Rais wa Baraza la Maaskofu na kumpatia jina la Kanisa la Mtakatifu Rufina. Hawa wote ni makardinali na maaskofu wahudumu wa karibu na Papa katika utume wake wa Kanisa.

02 May 2020, 08:11