Tafuta

Vatican News
Baada ya kurudi katika vyombo vya usafiri je na barabarani, Padre Lombardi anauliza swali je! tutarudi namna gani kesho kutwa kukutana katika barabara au Metro? Baada ya kurudi katika vyombo vya usafiri je na barabarani, Padre Lombardi anauliza swali je! tutarudi namna gani kesho kutwa kukutana katika barabara au Metro?  

Padre Lombardi:Tutakutana tena kwa mtazamo upi?

Padre Lombardi ameanza makala mpya zinazotazama hali halisi ya baada ya janga na wakati ujao unatotusubiri.Yesu hakujionesha umungu wake kwa njia ya mitandao ya kidijitali,bali alijifanya mwili ili kwamba tuweze kukutana. Yesu alituambia kuwa yeye yupo na anatusubiri kule.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mzunguko mpya wa makala za Padre Federico Lombardi, kuhusiana na mtazamo wa hali halisi hasa ya wakati ujao mara baada ya janga, anaanza kwa tfakari moja aliyoisoma kwa siku hizi kutoka kwa mchambuzi mmoja wa kirusi aliyendika kuwa: “uhusiano rahisi kati ya watu ni jambo muhimu duniani!” Wazo hili pia limemfanya akumbuke akilini mwake, juu ya wimbo mzuri wenye kujaa furaha wa miaka iliyopita hivi ambao uliotolewa na kikundi kimoja cha vijana waliokuwa wanahamasisha urafiki na udugu kati ya watu. Wimbo huo ulikuwa na jina: “Viva la gente!” yaani  "watu hoyee”.  Padre Lombardi kwa maana hii anafikiri kuwa bado kuna ambaye anaukumbuka wimbo huo. Wimbo huo  anaandika ulikuwa unaelezea juu ya watu tunaokutana nao kila siku wakienda kazini na zaidi ulikuwa unasema: “ikiwa watu wangeweza kuwatazama watu wengine kwa wema, tungeweza kuwa na watu wachache walio wagumu na kuwa na watu wenye moyo mkuu zaidi…” na kwa maana hiyo anasisitiza Padre Lombardi kwamba wimbo huo ulikuwa unaamsha hisia nzuri za hekima na zenye uchanya.

Padre Lombardi katika makala hii kuhusu baada ya janga, anabainisha alivyokuwa anaufikiria sana kwenye miaka ya mwisho  wakati akitembea barabarani, akikutana na watu wengi ambao wanangaika na kukimbizana, wengine walio jifungia binafsi na wengine wengi wakiwa na nyuzi zinazo chomoza kwenye masikioni mwao, ambao walikuwa wamo kilindini kabisa kwenye skrini ya simu zao za mkononi au wakiongea hewani kwa sauti kubwa , ni nani anajua nani, bila kujali watu ambao walikuwa kwenye Bus  au karibu na hatua ndogo nao.Kwa upande wake alikuwa akionesha ile shauku ya kuwatazama wengine kwa uaminifu na uangalifu jambo ambalo lilikuwa limekwisha geuka kuwa nadra na  tendo la kuongezeka kwa njia mpya za mawasiliano katika maisha ya kila siku zimelikwa zimefanya kuwa wageni karibu nasi.

Baada ya wiki kadhaa tukiwa ndani ya nyumba zetu, tumetengwa, Padre Lombardi anahisi  ile shauku ya kukutana kwa upya katika barabara na sura tofauti. Ni tumaini lake lakini kwamba kabla au baadaye Mungu akipende, inawezakana kutembea hata bila barakooa bila vitengenishi vya vyoo na matarajio yake ya kuweza kubadilishana salam za upendo au hata kwa njia ya tabasamu ya kweli. Wengi sana kati yetu Padre Lombardi anathibitisha kwamba, kwa miezi hii wamefanya uzoefu na kwa mshangao chanya wa uwezekano unaotolewa na mawasiliano ya kidijitali na ni tumaini ya kwamba, njia hii inaweza kuwa tunu hata kwa wakati ujao, lakini tendo la kuzidisha muda mrefu wa upweke na kujitenga, umefanya kutambua kuwa njia hizi  hazitoshi.

Je tutarudi namna gani kesho kutwa kukutana katika baraba au Metro? Je tutarudia kukusanyika kwa utulivu katika nafasi za kawaida katika miji yetu? Tutakuwa na woga au tuhuma, au kwa msaada wa hekima inayotarajiwa ya wanasayansi na watawala, kuweza  kweli kudhibiti usawa na busara na shauku ya kuweka upya ule ubora wa umoja wa kuishi kila siku ambao  kama tulivyosema hapo mwanzoni “ndiyo muhimu zaidi katika ulimwenguni ”, nyumba ya buibui ya ulimwengu wa mwanadamu yenyewe? Je! Tutagundua (zaidi au kidogo kuliko hapo awali?) Ya kuwa sisi sote ni familia ya wanadamu katika safari huku tukitembea katika nyumba ya pamoja na ambayo ndiyo sayari yetu pekee ya dunia?

Kwa sasa ambapo janga hili limetufanya kuwa na uzoefu wa shida ya utandawazi ambayo sisi sote tutalazimika kuzingatia katika siku zijazo, tutaweza kuwa na mwamko wa kuwa na kasi kwa udugu kati ya watu mbali na zaidi ya mipaka, ukarimu mzuri na kufanya udadizi katika utofauti, wa matumaini ya kuishi pamoja katika ulimwengu wa amani? Je! Tutaishije miili yetu na tutaionaje ile ya wengine? Njia inayowezekana ya kueneza, hatari ya kuwa mwangalifu, au usemi wa roho ya dada au kaka? Kwa sababu hii kimsingi ni kila mwili wa mwanadamu, ni udhihirisho kamili wa roho ya pekee, anayestahili, mwenye thamani, kiumbe wa Mungu, sura ya Mungu…

Ni jinsi gani ya kupendeza kwa sauti, wimbo katika hatua na zaidi tabasamu yote ya wapendwa! ... anasisitiza Padre Lombardi, aidha anauliza tena: "Lakini zaidi, Je! Hii haifai kutumika kwa watu wote ambao tunakutana nao? Kwa maana hiyo, tutaweza kupata kwa upya ule uhuru kutokana na virusi vya corona  pia kutusaidia kuondoa virusi vingine mwilini na roho ambavyo vinatuzuia kuona na kukutana na hazina ambayo iko kwenye roho ya mwingine, au tutakuwa na kibinafsi zaidi? Teknolojia ya kidijitali inaweza kuelekeza na kutumika kwa uhusiano wetu, lakini uwepo kwa pande zote za watu, miili yao kama uwazi wa roho, ukaribu wao na mkutano wao, vinabaki kuwa sehemu iliyo muhimu sana na  ya uhakika na mahali pa kumbukumbu ya uzoefu wetu katika safari zetu.

Yesu hakuwa udhihirisho dhahiri wa Mungu kwa njia ya kidijitali, bali kwa njia ya mwili wake, kwa dhati ili tuweze kukutana naye. Na Yesu alituambia kuwa yupo na anatusubiri kule, kwa masikini (na ambaye siyo masikini kwa njia fulani, anajua au hapana?), Na kwamba kwa njia ya kuonana uso kwa uso wa mwingine tunaweza na lazima tujue jinsi ya kutambua sura yake, Padre Lombardi anasisitiza. Na kwa kuhitimisha makala hii anauliza. Je ni kwa  mtazamo gani, kwa moyo gani,na tabasamu gani tutarudi kutembea barabarani na kuvuka njia za watu wengi, ambao ingawa haijulikani katika miezi michache iliyopita wamekosekana,na ni kama sisi wamehisi shauku ya kukutana kwa upya kwenye barabara za kila siku za maisha yao, za ulimwengu wetu wa kawaida?

 

02 May 2020, 14:30