Tafuta

Vatican News

Mtakatifu Yohane Paulo II na wakristo wa Mashariki!

Baraza la Makanisa ya Mashariki wametengeneza video ya kuonesha matukio muhimu na ambayo yanaunda historia ya maisha yao katika utume wa Mtakatifu Yohane Paulo II.Ni katika muktadha wa kumbukizi la miaka 100 tangu kuzaliwa kwake(1920-2020).

Katika video inashuhudia imani kuwa ya kuwa "huwezi kupumua kama mkristo na zaidi kama mkatoliki na pafu moja, lazima kuwa na mapafu mawili, lile la mashariki na magharibi".

Na ndiyo moyo wa video ambayo katika fursa ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II(920-2020),imetengenezwa kwa ajili ya kutoa heshima hiyo kwa mujibu wa Baraza la Makanisa ya Mashariki.

Muziki wa kiliturujia  unaoisikika ni wa utamaduni wa makanisa ya Mashariki ambao juu yake zinapita picha ambazo zilipigwa na kutolewa na huduma ya wapiga picha Vatican. Hata hivyo picha hizo zinaonyesha juu ya ziara ya Papa Yohane Paulo II katika Nchi Takatifu na kutangazwa kwa Gombo la Sheria ya Makanisa ya Mashariki; Wosia wa Kitume kwa ajili ya Maelekezo ya Nchi za Mashariki na kutangazwa kwa Watakatifu Cirily na Methodius ambao ni watakatifu, Wasimamizi wa Ulaya na Sinodi Maalum ya Lebanon. 

Hatimaye picha zinaonesha hata heshima ya watu wa Mashariki wakiwa wamezungukia jeneza la Mtakatifu Yohane Paulo II.

18 May 2020, 15:57