Tafuta

Vatican News
Matumaini mapya baada ya janga la virusi vya corona ndiyo nuru ya ushindi/ Matumaini mapya baada ya janga la virusi vya corona ndiyo nuru ya ushindi/ 

Lipo Kanisa nyenyekevu kwa ajili ya ubinadamu uliojaribiwa!

Katika makala ya mwisho ya Padre Lombardi kuhusu wakati ujao unaotusubiri baada ya janga:swali lake anauliza je,tutakuwa jumuiya yenye uwezo wa kusindikizana kidugu kwa upendo na wema?

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika makala ya mwisho ya Padre Lombardi kuhusu wakati ujao unaotusubiri baada ya janga anaanza na swali kuwa: Je tutakuwa jumuiya yenye uwezo wa kusindikizana kidugu kwa upendo na wema? Kwa kuanza kufafanua amesema “Wakati wa kuhitimisha Jubilei kubwa ya  mwaka 2000 na ambayo alikuwa ameiishi kwa kina na kuwaalika watu wa Mungu waiishi kama fursa muhimu ya neema ya Kristo na historia ya ubinadamu, Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa ameandika kwa Kanisa zima barua yake ya kitume nzuri sana iliyokuwa inaongozwa na kauli mbiu “ Mwanzo wa Milenia ya Tatu”.

Wosia huo ulikuwa na mwangwi wa maneno ya Yesu akimwambia Petro “ ‘Duc in altum’…peleka mbele mashua na mkatupe nyavu zenu mpate kuvua samaki” (Lk,5,4). Papa Yohane Paulo II alikuwa anawaalika watu wa Mungu wafanye kumbu kumbu ya wakati iliopita, ili kuishi kwa kutoa shukrani ya wakati uliopo, na  kujifungulia matumaini ya wakati ujao, kwa kuwa Yesu Kristo ni wa leo, jana na daima. Padre Lombardi anasema, na kama tunavyotambua pia  Papa Francisko ameendeleza mada hii ambayo tangu mwanzo wa upapa wake yanajionesha  katika maneno ya “Kanisa linalotoka nje”, yaani Kanisa la kuinjilisha linaloongozwa na Roho Mtakatifu kutoka kwa Kristo Mfufuka.

Katika tafakari yake ya mwisho, Padre Federico Lombardi ambaye amejikita kusindikiza katika kipindi hiki cha Janga la corona kwa tafakari za kina hasa kwa waamini na wasio waamini ambao wamelazimika kutengwa na kukaa ndani ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona kila wiki, zimekuwa za kusisimua na zenye kuongoza katika hali halisi ya kuwa na matumaini ya wakati ujao baada ya mgogoro wa covid-19. Padre Lombardi anasema, jioni ya tarehe 12 Oktoba 2012 Papa Mstaafu Benedikto XVI alikuwa ametoa hotuba ya kuaga  chini ya mtazamo mzuri wa mwezi, kwa umati uliokuwa umekusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro siku moja baada ya ufunguzi wa Mkutano.

Papa Mstaafu Benedikto XVI kwa mtazamo wake ukiwa kuwaumeinuliwa juu, alitoa tafakari iliyoshangaza sana, kwa sababu hakuna aliyetarajia kusikia kauli yake lakini kwa kuongozwa na imani  na unyenyekevu mkuu aliweza kutamka juu ya kuhitimisha hduma yake ya kipapa. Alikuwa amekumbuka jinsi  gani miaka 50 iliyokuwa imetangulia, Kanisa lilikuwa limefanya uzoefu wa dhambi, yaani kama magugu yaliyokuwa yamechanganywa na ngano katika shamba, dhoruba na upepo tofauti, moto wa roho mtakatifu, moto wa Kristo. Lakini kwamba ulikuwa ni moto ambao haukuwa unaunguza badala yake wenye unyenyekevu na wa ukimya, moto mdogo ambao unakuza karama za wema na upendo na ambavyo vyote vinaangaza ulimwengu na kushuhudia uwepo wake na sisi.

Padre Lombardi akiendelea na tafakari hiyo, anasema kuwa ikiwa tunakaribia siku ya Petentekoste, anafikiria kwa upya yale  maneno ya mapapa watatu wa Milenia ya Tatu. Katika hali halisi, Milenia Mpya ambayo tayari tulikwisha ingia miaka 20 iliyopita, na ambayo kwa haikujionyesha kipindi kwa ujumla maendeleo angavu kwa ubinadamu. Hii ni kwa sababu anataja matukio ambayo yamejitokeza. Awali ya yote Milenia ilifunguliwa na mashambulizi ya kigaidi kunako tarehe 11 Septemba 2001, na vita vya ghuba, baadaye tumeona mgomgoro mkubwa wa kiuchumi, na vita vya ulimwengu vilivyogawanyika vipande vipande, uharibifu mkubwa wa nchi ya Siria na Libia, uongezeko la uharibifu na mgogoro wa mazingira, kwa wastani  matatizo mengi, na sasa janga la kidunia lenye kuwa na  matokeo yake hasi na ni uzoefu ambao umekuwa katika kipindi cha uongozi wa mapapa wa nyakati zetu.

Padre Lombardi anasema licha ya hayo mafanikio lakini hayakukosekana kama yale ya kisayansi, maendeleo ya kiafya, mafunzo na njia za mawasiliano ambazo bila hizo isingekuwa rahisi kutambua na kujua kinachoendelea duniani na tathimini za haraka zilizo hasi au chanya. Pamoja na hayo hatuwezi kutozungatia pia  juu ya michakato ya  safari sahihi na uhakika wa ubinadamu katika kuelekea ubora, ambainisha. Uzoefu wa janga , hata kama tutashinda ni kwamba tumefanya uzoefu wa pamoja ambao unaonyesha ni jinsi ya kutokuwa na usalama, pia  matatizo ya kiserikali, katika mchakato wa kutembea daima na ugumu kwa jamii ya sasa. Hatujuhi kiukweli wakati ujao  kama uzoefu huu utakuwa fursa za kukua katika mshikamno au mivutano mipya ya kimatifa na ya ndani na kuyumba kwa kijamii. Labda yote mawili yatachanganyikana kama ngano na magugu.

Kanisa katika mwanzo wa Milenia kwa mtazamao wa macho ya kibinadamu  halina nguvu kwa sababu imani yake imewekwa katika majaribu na kusababisha jangwa la kiroho katika nyakati zetu. Uaminifu wake umewekwa katika majaribu ya kunyenyekezwa na kivuli cha kashfa. Historia inaendelea na Kanisa linaendelea kujifunua katika njia moja ya nguvu ya kweli ni imani katika Kristo Mfufuka na zawadi ya Roho Mtakatifu. Ni  chombo dhaifu cha udongo ambacho lakini ndani mwake kinahifadhi tunu ya nguvu ya maisha ambayo yanakwenda zaidi ya kifo.

Maswali, anazidi kuuliza: Je tutakuwa Kanisa nyenyekevu lenye uwezo wa kisindikiza kidugu ubinadamu uliojaribiwa, kwa upendo na wema? Upendo unaosambazwa, unaoongozwa hata na haki na nguvu ya kijamii katika kutafuta na kupata njia za ustawi wa pamoja na maisha yaliyo bora? Ni Kanisa linaloosha miguu katika wakati wetu, kama asemavyo Papa Francisko? Padre Lombardi anasema, Lakini kumbuka  “Nje ya pwani, katika baharini bado na daima wapo wasiojulikana kwetu sisi, lakini  ambao kamwe siyo wageni kwa upendo wa Mungu.

Katika sala ya Pentekoste, tunaomba roho Mtakatifu kama baba wa maskini, mwanga wa mioyo na kama msadizi na mfariji, kama nguvu inayo okoa dhidi ya dhambi, kufunga majeraha, kupasha joto penye baridi na kuonyesha njia kilichopotea. Kwa maana hiyo tuhahitaji kutoa nafasi iliyo wazi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu,kusubiri na shauku, ambainisha Padre Lombardi.

18 May 2020, 10:03