Tafuta

2020.05.23 Toleo la kitabu:Tofauti na Tulioungana kimetolewa katika Duka la vitabu Vatican. 2020.05.23 Toleo la kitabu:Tofauti na Tulioungana kimetolewa katika Duka la vitabu Vatican. 

Tofauti na tumeungana.Utajiri wetu wa kweli ni uhusiano na sio kwa ajili ya vitu!

Katika tafakari nyingi za Papa Francisko zinazohusiana na mahusiano ya kibinadamu anabainisha kuwa msingi wa kila mawasiliano na uhusiano wa binadamu upo uwezekano wa kumsikiliza mwingine.Hata hivyo katika kitabu kilichopewa jina:"Tofauti na tumeungana".Utajiri wetu wa kweli ni uhusiano na sio kwa ajili ya vitu vya mwili" ni fursa ya kigundua kwa dhati uhusiano huo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Toleo jipya la kitabu limetolewa katika Duka la Vitabu, Vatican(LEV), chanye kichwa cha habari “ tofauti na tumeungana” ambacho  kinakusanya maandishi na hotuba za Papa Francisko kuhusu mahusiano ya kibinadamu, ambayo ni katika mkusanyiko wa katekesi zake kuhusu familia. Kitabu hicho ni cha tatu kati ya mfululizo wa vitabu vingine viwili kama vile  'kubadilishana zawadi' ambavyo utangulizi wake umetiwa sahini na Patriaki Bartolomeo I wa Kiekumene huko Costantinople, na  Patriaki Kirill wa Moscow nchini Urusi. Katika fursa ya maandiko ya Papa, utangulizi wake umeandaliwa na kiongozi wa kikristo, Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, Mkuu wa Kanisa la Uingereza na Kiongozi Mkuu wa Umoja wa waanglikani ulimwenguni. Katika utangulizi huo, yeye amesisitiza sawa na mawazo ya  Papa Francisko kuhusu mada ya uhusiano wa kibinadamu ambao unatambuliwa kwa jinsi gani ni mzuri na wenye kuleta matunda hasa ule unasimika mzizi wake juu ya upendo ambao Mungu anao kwa ajili yetu.

Kuwa na mtazamo wa Yesu

Wengi waliokutana na Yesu katika njia zao huko Palestina waliangazwa na mtazamo wake, wenye ujazo wa upendo kwa kila mtu. “Tufikirie wito wa Matayo (aliyetazamwa kwa upendeleo pamoja na huruma); mazungumzo ya usiku na Nikodemu, au akiwa na msamaria katika kisima cha Yakobo, na labda hata mtazmo ule wa haraka zaidi wa mwanamke mkananayo na Zakayo. Kwa hakika mtazamo ule wa Yesu ndiyo ambao aliutoa katika shavu la Yuda akimwita 'rafiki'. Ndiyo tazamo ambao anamwelekea Petro wakati jogoo anawika na hata kama inakuwa ngumu kutambua hilo! Ndiyo mtazamo ambao kwa kimya alikuwa anamtazamo Mfalme Erode ambaye alikuwa akisubiri kutoka kwake ishara ya miujiza kabla ya kumtuma kwa Pilato. Hata katika mazungumzo na Jaji mkuu wa kirumi , Yesu alikuwa na mtazamo wa upendo. Katika mtazamo wa  Yesu ni kuwa na utambuzi wa imani ya kikristo ambayo inasimika mzizi wake kutokana na maneno ambayo kama Papa Francisko anathibitisha  kuwa "Yesu ni asili ya Mungu na Mungu ni upendo". Msingi huo anaandika Papa “ni dhihirisho la matokeo mengi na mabadiliko yote kwa namna ya kukaa mkristo katika ulimwengu”

Kuwasiliana na kusikiliza

Katika msingi wa kila mawasiliano na uhusiano wa binadamu upo uwezekano wa kumsikiliza mwingine. “Bila mtazamo wa upendo, mawasiliano ya binadamu na mazungumzo kati ya mtu na mtu, kwa urahisi Papa anabainisha, inawezekana  kuwa maneno ya kijuu juu. Na hiyo ina maana ya kwamba mtazamo ule unajionesha kwamba kuna ulegevu wa masuala mengine ya  kutetemesha na ambao hauna kiini kinachostahili cha mjadala. Kwa maana hiyo, Papa anasisitiza kuwa lazima kujua namna ya kufanya “uchaguzi wa Mtakatifu Kardinali John Henry Newman”. Tafakari lake linajikita kwa namna ya pekee juu ya ukuu wa hisia na makubaliano ya moyo ambao unayo nafasi muhimu kulingana na ile ya sababu, ili mtu aweze kweli kuzungumza na uzoefu wa imani.

Magharibi itambue Mashariki maana ya shairi

Katika kitabu ambacho kimetolewa  siku ya kumbukizi la mwaka wa 25 wa Wosia wa Ut unum sint  kuhusu ukumene  wa Mtakatifu Yohane Paulo II alioutangaza kunako terehe 25, Mei 1995, Papa Francisko kwa namna ya pekee anasisitiza  juu ya tukio la “kijana tajiri” ambaye alimwomba Yesu afanye nini ili kurithi ufalme wa mbingu.  Papa anakumbuka kila sehemu na kufafanua ule uthabiti ambao upo katika Injili ya Marko tu. Mwinjili anaandika kuwa Yesu alimtazama na kumpenda. Hasa katika jamii za Magharibi, Papa anasema neno kutazama , tabia ya kutafakari utafikiri siyo  ya kawaida, kwa sababu imepotea katika nafasi za kila siku na maisha ya kila siku. Hakuna anayemtazama mwingine na zaidi ni kumbagua kwa maana ya kuhisi kama ni hatari. Kwa kufikiria hiyo anarudia kuwa na kumbu kumbu ya hali halisi katika ziara yake barani Asia mwezi Novemba mwaka jana na ambamo aliwataka  watu wa Mashariki wawe na maana ya wimbo mzuri au shairi hasa akizingatia sehemu nzuri za kutafakari  kutulia na kujifungua binafsi na wengine.

Mtazamo wa Mungu uwe kwetu daima

Mwishowe, Papa anabainisha kuwa kupenda kunamaanisha hata kuthubutu katika hatari. Wakati anamtazama yule kijana aliye mbele yake, Yesu hakumtazama machoni ili atambua alama za udhaifu wake, lakini alimfikiria kana kwamba ametoka mikononi mwa Mungu Baba na alifurahi kwa uwepo wake. Alimpenda kwa dhati  na alimwita kama vile anatoa gerezani na majeraha ya zamani kwa ajili ya mustakabali wa ukamilifu. Na kwa maana hiyo aliweza kujibu swali lake juu ya uwezekano wa uzima wa milele. Tuombe nasi ili mtazamo wa Mungu uweze kuwa juu ya  maisha yetu kila wakati na sisi sote kwa mara nyingine tena tunaweza kuingia katika  uhusiano na kuwasiliana na watu wengine. Tuwe na mtazamo kama wa Yesu anayetutazama kwa macho ya upendo na ukarimu hadi kujitoa mwenyewe kwa jili yetu, Papa anasema.

25 May 2020, 16:13