Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 23 Mei 2020 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bi Maria Fernanda Silva, Balozi mpya wa Argentina mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 23 Mei 2020 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bi Maria Fernanda Silva, Balozi mpya wa Argentina mjini Vatican. 

Balozi wa Argentina awasilisha hati za utambulisho mjini Vatican.

Bi María Fernanda Silva alizaliwa tarehe 20 Desemba 1965. Alianza shughuli za kidiplomasia tarehe Mosi, Januari 1993 na tangu wakati huo amebahatika kuwa mwakilishi wa Argentina, kwenye Tume ya Uchumi Kanda ya Amerika ya Kusini na Caribbean. Amewahi kuwa Katibu Kwenye Ubalozi wa Chile, Katibu wa Kurugenzi ya Ulaya ya Magharibi, Mshauri kwenye Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi, tarehe 23 Mei 2020 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bi María Fernanda Silva, Balozi mpya wa Argentina mjini Vatican. Bi María Fernanda Silva alizaliwa tarehe 20 Desemba 1965. Alianza shughuli za kidiplomasia tarehe Mosi, Januari 1993 na tangu wakati huo amebahatika kuwa mwakilishi wa Argentina, kwenye Tume ya Uchumi Kanda ya Amerika ya Kusini na Caribbean, “The Economic Regional Commission for Latin America and the Caribbean”, ECLAC/CEPAL. Amewahi kuwa Katibu Kwenye Ubalozi wa Chile, Katibu wa Kurugenzi ya Ulaya ya Magharibi, Mshauri kwenye Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Amewahi pia kuwa Katibu Msaidizi wa Kurugenzi ya Masuala ya Kikanda. Kuanzia Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Masuala ya Kisiasa nchini Venezuela.

Kunako mwaka 2012 akateuliwa kuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ya Amerika ya Kusini “Union of South American Nations”, “União de Nações Sul-Americanas, UNASUL/UNASUR. Makao Makuu ya Umoja huu yako huko Quito. Mwezo Oktoba 2014 akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Masuala ya Kisiasa Amerika ya Kusini. Kuanzia mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Waziri maalum wa masuala ya uhusiano na Vatican. Mwaka 2016 akateuliwa kuwa Mwakilishi Msaidizi wa Argentina katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao makuu mjini Roma. Haya ni Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO; Shirika la Maendeleo ya Kilimo, IFAD pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP. Tarehe 23 Mei 2020 amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko pamoja na kupata nafasi ya kukutana na viongozi waandamizi mjini Vatican, tayari kuanza utume wake wa Kidiplomasia!

Argentina: Hati za Utambulisho

 

 

 

25 May 2020, 13:15