Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Noel Andrew Rucastle kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Oudtshoorn, Afrika ya Kusini. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Noel Andrew Rucastle kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Oudtshoorn, Afrika ya Kusini. 

Mh. Pd. Noel Andrew Rucastle: Askofu Mpya Jimbo la Oudtshoorn!

Askofu mteule Noel Andrew Rucastle alizaliwa tarehe 22 Aprili 1968 huko Kimberley. Tarehe 14 Julai 2000 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuingizwa katika Jimbo kuu la Cape Town, Afrika ya Kusini. Tangu baada ya Upadrisho amebahatika kufanya utume katika Parokia mbali mbali Jimboni humo. Kati ya Mwaka 2018 na mwaka2020 alikuwa Paroko wa Parokia ya "Our Lady of Fatima".

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa Sana Padre Noel Andrew Rucastle kutoka Jimbo Katoliki la Oudtshoorn, Afrika ya Kusini, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Oudtshoorn. Askofu mteule Noel Andrew Rucastle alizaliwa tarehe 22 Aprili 1968 huko Kimberley. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 14 Julai 2000 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuingizwa katika Jimbo kuu la Cape Town, Afrika ya Kusini. Tangu baada ya Upadrisho amebahatika kufanya utume katika Parokia mbali mbali Jimboni humo kama: Paroko-usu na Msimamizi wa Parokia ya Mtakatifu Anthony wa Padua kati ya Mwaka 2003 hadi mwaka 2006 huko Kraaifontein.

Kati ya Mwaka 2006 hadi Mwaka 2010 alipelekwa na uongozi wa Jimbo kujiendeleza zaidi na hatimaye kufanikiwa kujipatia Shahada ya Uzamili kuhusu Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, nchini Canada. Baada ya kurejea nchini Afrika ya Kusini kati ya Mwaka 2012 hadi mwaka 2018 aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Parokia ya “St. Mary’s Cathedral pamoja na kuwa ni Wakili wa Jimbo kuu la Cape Town rangu mwaka 2011 hadi kuteuliwa kwake mwaka 2020. Kati ya Mwaka 2012 hadi Mwaka 2018 aliteuliwa kuwa kuwa Paroko wa Parokia ya “St. Anthony” iliyoko huko Hout Bay. Hatimaye, kati ya Mwaka 2018 hadi 2020 aliteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya “Our Lady of Fatima” huko Bellville.

Afrika ya Kusini
04 May 2020, 13:23