Tafuta

Vatican News
Papa Francisko katika ziara ya bunge  la Umoja wa Ulaya huko Strasburg. Papa Francisko katika ziara ya bunge la Umoja wa Ulaya huko Strasburg. 

Kurudi katika ndoto za Mababa Waanzilishi

Katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ulaya inayoadhimshwa kila tarehe 9 Mei na ambapo mwaka huu itaadhimisha katika roho tofauti,Dk.Gissotti katika makala yake aliyoipa jina “Kurudi katika ndoto ya Mababa Waanzilishi”anakazia juu ya mshikamano kwa mujibu wa mawazo ya kinabii ya baadhi ya viongozi kama Papa Francisko anayekazia mshikamano wa dhati.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican  

Katika saa ambayo ni ngumu kwa upande wa Ulaya kulinganisha na baada ya vita ya Pili ya Dunia, inatakiwa kurudi katika uasili wa mpango wa kiulaya ambao unaweza kusaidia kupata mwamko mpya kwa ajili ya Bara zima la kizamani. Ndiyo ndoto ya Mababa waanzilishi kama vile Papa Fransiko aliyefafanua kama ndoto ya dhati inayoitwa mshikamano. Ndivyo anavyoandika katika makala yake mwandishi wa habari wa Vatican News, Dk. Alessandro Gissotti katika makala aliyoipa jina “ritornare al sogno dei Padri Fondatori”, yaani “Kurudi katika ndoto ya Mababa Waanzilishi”. Tarehe 9 Mei ijayo kama kila mwaka Dk Gissotti anaandika, ni maadhimisho ya Siku ya Ulaya ambapo kwa mwaka huu  unahitimisha miaka 35 japokuwa kwa namna ya pekee itakuwa siku yenye roho tofauti, kwa sababu siku hii itakuwa sambamba na hatua za kwanza  katika harakati ya kujaribu  kurudia maisha ya ukawaida na Nchi nyingine labda ndiyo zitakuwa zinaendelea bado kuwa karantini kwa sababu ya maambukizi ya  Covid-19.

Kwa hakika sherehe hizi zinazoangukia katika kipindi cha janga,  kwa ajili ya Ulaya baada ya Vita ya Pili ya Dunia, inaweza kuwakilisha fursa ya kujikita kutafakari juu ya utambulisho na utume wa Nyumba Yetu ya Ulaya, anaandika Dk. Gissotti. Kwa mujibu wake kuanzia na Siku hii ya tarehe 9 Mei na  ambayo  anaandika inawezekana ni wachache kati ya raia wa Ulaya kuitambua kama ni  siku yao binafsi na zaidi si hajabu  kidogo wanajiuliza ni kwa nini iliachaguliwa siku ya tukio hilo. Kwa kutaka kufafanua zaidi Dk. Gissotti anaandika:  "tarehe  9 Mei 1950  inakumbuwa  kwa sababu hii itakuwa ni kuadhimisha miaka 70 tangu  aliyekuwa waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa Robert Schuman  wa wakati ule alipotoa hotuba ya kukumbukwa na ambayo alipendekeza kuundwa kwa uzalishaji wa Makaa ya mawe na uzalishaji wa chuma Ulaya (ECSC)". Hii ilikuwa ni hatua ya kwanza kuelekea  njia ambayo, kupitia mlolongo wa taasisi za bara, ingeongoza kwa miaka arobaini baada ya kuzaliwa kwa Umoja wa Ulaya.  Umuhimu wa taarifa hiyo ni wa kushangaza kwa kipindi cha sasa, anabainisha Dk. Gissotti, hii ina maana kwamba,  Schuman, kiukweli, alikuwa bado anaona machoni mwake ile picha za uharibifu uliosababishwa na vita vilivyoharibu Ulaya na dunia na alikuwa akionya kwamba amani isingeweza kulindwa  au kupatika ikiwa siyo kwa  njia za juhudi za ubunifu, usawa dhidi vitisho vya hatari.

Amani na mshikamano. Schuman alikuwa akithibitisha kuwa Ulaya kwa kuona njia ambayo ingekuwa imejitokeza katika miongo kadhaa iliyofuata isingeweza kufanywa mara moja, wala kujijenga kwa pamoja badala yake Ulaya ingeweza kupata mafanikio halisi ambayo kwanza itaundwa  kwa njia ya mshikamano wa wa kweli. Akizungumzia juu ya malengo msingi wa  Uzalishaji wa makaa mawe na  uzalishaji wa chuma (ECSC), kwanza kabisa  Ufaransa na Ujerumani alisisitiza  kuwa uzalishaji huo ulikuwa utolewe katika  ulimwengu wote bila ubaguzi au kutengwa ili kuchangia kuongezeka kwa kiwango cha maisha na maendeleo ya shughuli za amani.

Dk. Gissotti anaongeza kuandika kuwa uwezo wa unabii wa maneno hayo ulikuwa kwamba, hata baada ya miaka mingi, kwenye Baraza la Ulaya la Milano kunako Juni 1985 waliuchukuliwa kama eneo muhimu la kufanya  kumbukumbu  ya Siku ya Ulaya ambayo, inakwenda sambamba na tarehe ambayo Schuman alitoa hotuba yake maarufu. Ukaribu wa  maadhimisho haya, katika hali ambayo inaweka wasiwasi juu ya utulivu wa ujenzi wa Ulaya anasema Dk. Gissoti, unatukumbusha kwamba mengi zaidi yanaweza kutufundisha kama ya “Mababa Waanzilishi” ambao wameweza kujibu dharura tofauti, lakini siyo kubwa kama ilivyo ya leo ambayo wanaitwa  viongozi wa Jumuiya ya Ulaya kukabiliana nayo. Wanasiasa wenye malengo na wa kweli, wakikumbuka maneno ya Joseph Ratzinger, (yaani Papa Mstaafu Benedikto XVI) ambaye alikuwa anawashauri kuishi siasa iliyo safi na ambayo inatakiwa iwe ya kimaadili.

Kurudi katika mizizi na thamani msingi zilizounda Ulaya ndiyo wito ambao Papa Francisko, kama Papa wa kwanza hasiye wa mzaliwa wa Ulaya baada ya karne nyingi ameendelea kuweka umakini wake kwa viongozi na watu wote wa Ulaya na zaidi katika ujumbe wake  wa mwisho ulioshangaza waamini wengi wa Urbi et Orbi ya Pasaka mwaka huu. “Baada ya Vita ya Pili ya Dunia, bara hili limeweza kuonekana baraka  nyingi za dhati  katika roho ya mshikamano ambao umewezesha kushinda vikwazo vya wakati uliopita”. Vurusi vya  kizamani vya migawanyo na ubinafsi, ambao unarudi, chanjo yake daima ya dhati ni mshikamano au kwa kutoa neno ambalo anapenda Papa “udugu wa kibinadamu” ( Papa Francisko urbi et Orbi -Pasaka. Kuna haja ya kurudi katika kumbu kumbu ili kukabiliana na wakati uliopo kwa kufanya mikakati na mipango ya wakati ujao na zaidi katika nyakati ambazo zinaonesha ukosefu wa uhakika. Hata katika ziara zake za Kitume barani Ulaya na daima katika nchi zilizo mbali na kitovu cha kisiasa na kiuchumi, kwa mfano wa ziara yake ya kwanza nchini Albania na ya mwisho nchini Romania. Dk. Gissotti anaongeza, labda njia nzuri zaidi ambayo alihimiza ni ile ya kurudi kwenye mizizi, katika nyayo za  Papa mwingine mkubwa wa Ulaya kama Papa Yohane  Paulo II.

Tarehe 6 Mei 20216 akihutubia kwa wakuu wa Taasisi za Ulaya, Papa alikuwa alikumbusha wa kutumia maneno ya  Elie Wiesel, kuwa kuna haja ya Ulaya kwamba katika Ulaya tunahitaji uhamishaji wa kumbukumbu huko. Hii, alisisitiza, akinukuu maneno ya waathirika wa kambi za mateso za Kinazi, “sio kwamba hautaturuhusu tu kufanya makosa yale yale ya zamani, lakini pia itatupatia ule ufikiaji wa kupata ambao ulisaidia watu wetu kuvuka barabara kuu za kihistoria ambazo walikuwa wakienda kukutana nazo”. Ameandika Dk. Gissotti. Aidha akiendelea, ndoto ya Papa Francisko kwa ajili ya Ulaya ni ile ya Mababa Waanzilishi. Ni ndoto ambayo inatakiwa kurudi kama alivyosema wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ndege wakati anatoka ziara nchini Romania kunako tarehe 2 Juni iliyopita. Ndoto hiyo inaitwa “mshikamano” ambao leo hii unahitajika sana kuliko awali katika “kusasisha wazo la Ulaya”.

Katika fursa ya maadhimisho ya maiak 60 ya Mikataba ya Roma, akikutana na Viongozi wa Nchi na serikali ya Nchi za Umoja wa Ulaya, Papa Francisko alisisitza kuwa Ulaya inapata matumaini katika mshikamano ambao pia ni wa dhati na dawa dhidi ya mitindo ya sisasa ya ubinafsi wa watu. “Mshikamano alionya siyo kama kufanya mapendekezo mema. Mshikamano una tabia ya kuwa na matendo na ishara za dhati” na alikumbusha kuwa “kuanzia katika mshikamano ndiyo lazima uwe njia  mpya ya kufikiria namna ya Ulaya”.

Hatimaye Dk. Gissotti anabainisha kuwa, ilikuwa ni tarehe 24 Machi 2017  ambapo Papa Francsiko alipotamka maneno hayo. Imepitia miaka mitatu tu na bado miezi mitatu ya mwisho iliyopita  inaonekana mzigo wao wa mateso, kifo na uchungu utafikiri unafanya kufafanan na  hotuba hiyo ionekane mbali zaidi kwa wakati. Lakini kiukweli  katika  shida tunayoishi kwa sasa inafanya iwe ya dharura zaidi, kwa sababu kama ilivyothibitisha miaka mitatu baadaye, akigusia Hati ya  Statio Orbis ya  27 Machi iliyopita: kwa hakika huu ni wakati wa mshikamano ambao hakuna mtu anaweza kujiokoa peke yake".

20 April 2020, 10:35