Tafuta

Vatican News
Uwanja wa Mtakatifu  Pietro, Vatican Uwanja wa Mtakatifu Pietro, Vatican 

Covid-19:kuna kesi mpya ya maambukizi mjini Vatican

Mfanyakazi katika makao makuu Vatican ameambukizwa na virusi.Mapema alikuwa tayari karantini na dalili na matokeo ya vipimo vya mwisho kabla ya kurudi kazini vimeonyesha chanya.

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa vyombo vya habari Vatican Dk.Matteo Bruni, alhamisi tarehe  30 Aprili 2020  ameeleza kuwa imethibitika kwa mara nyingine tena mfanyakazi mwingine wa Vatican na maambukizi ya Covidi19, na kufanya idadi kuwa  kumi na mmoja waliokwisha ambukizwa na virusi.

Hata hivyo mfanyakazi huyo alikuwa ameonyesha dalili za kwanza katikati ya mwezi Machi na kwa maana hiyo alianza mapema kujitenga kwa imani nyumbani. Na kufuatia na kupatikana na vipimo chanya ataendelea anabaki nyumbani kwake akiwa karantini.

30 April 2020, 16:39