Tafuta

Vatican News
2020.04.29 Jana na udugu ni kitabu kipatikacho katika E-book  kilichotangazwa na Askofu Mkuu Paglia. 2020.04.29 Jana na udugu ni kitabu kipatikacho katika E-book kilichotangazwa na Askofu Mkuu Paglia. 

Askofu Paglia:Baada ya janga,udugu ni njia pekee ya wakati ujao!

Katika kitabu cha hivi karibuni kupitia 'e-book' kuhusu“janga na udugu.Uwezo wa uhusiano wa kibinadamu unafungua tena wakati ujao",Askofu Mkuu Paglia,Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha na Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo II amezindua hatua ya“Mshikamano kama kinga ya virusi” na kutoa wito wa kuwa na maono ya viumbe ulimwengu kote.

Na Sr. Angela Rwezaula

Katika nyakati kwa sasa la janga limetuonesha udhaifu uliopo wa kila mmoja. Hata jamii na miundo ambayo tumejijengea ili kulinda maisha yetu, pamoja na fursa zote tulizo nafso, vyote hivyo matokeo yake ni kuwa dhaifu. Ni kwa mujibu wa Askofu mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha na Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo II.  Kwa upande wake anasema jibu moja liwezekanalo, la kutazama wakati ujao, ni lile la kujengwa juu ya udugu na juu ya mshikamano,  ikiwa na maana ya kuwa si katika maadili ya kikristo tu, lakini pia hata katika misingi ambayo inajikita juu ya kuishi kwa ubinadamu. Askofu Mkuu anasema hayo katika hekima ya kitabu alichokipatia jina “ Janga na Udugu.Nguvu za uhusiano wa kibinadamu kwa wakati ujao”.

Mjadala wa kimaadili na kiutamaduni kuhusu janga

Maandishi, kuanzia na yale ya hivi karibuni ya Taasisi hiyo anataka  kufungua mjadala wa kiadili na kitamaduni kuhusu baada ya janga na juu ya vigezo vya kuanza kwa upya. Dhana kuu ni “utandawazi wa udugu” na “kuenea kwa mshikamano wa kuzuia virusi”, kama anavyosisitiza Rais huyu wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha akihojiwa kwa njia ya simu na  Radio Vatican Italia. Askofu Mkuu Paglia anasema kwamba wakati Papa Francisko katika sala ya tarehe 27 Machi alisema kwamba, sisi sote tulikuwa tunakwenda mwendo kasi kuzidi kiasi, tukidhani tulikuwa wazima katika ulimwengu wa wagonjwa, alitukumbusha kwamba hatuna afya kabisa. Kulikuwa na virusi miongoni mwetu, kabla ya virusi vya corona, ambayo yeye amependa kuviita  ni virusi vya ubinafsi na upweke ambao kiukweli vilikuwa vimekwisha kudhoofisha jamii yetu.

Virusi vya corona vimeibua udhaifu wetu

Baada ya yote, virusi vya corona vimefanya kuibuka na kulipuka, udhaifu huo asili katika maumbile ya kila mmoja wetu, lakini hatutaki kuona, achilia mbali hata kuzingatia. Kwa maana hiyo  kuna haja ya kutumia akili ya wakati huu. Amesema Askofu Kuu Paglia. Ikiwa kiburi cha uweza wa kila mmoja wetu kitaendelea kuelekeza uchaguzi wetu, kuongoza maana ya maisha, mwisho ni dhahiri kwamba matunda ndiyo haya tumeona. Kwa hivyo ameongeza kusema kwamba ugonjwa huu unatuonyesha ukweli wa sisi ni nani. Virusi vya corona ni molekuli, hata hai, ya vimelea ambayo hata kwa kopi ya  jicho imepigisha kila mtu na kila kitu magoti, kuonyesha kwamba ikiwa udhaifu hautatambuliwa mapema mwisho  wake tunapata mateso. Na kwa maana hii basi hitaji la kulilia msaada, hitaji la kusaidiana, na kwa maana ya kusema inatosha  kwa kila ubinafsi, enzi kuu, kwa kila majitoleo, mwishowe yote hayo yapo katika maisha ya wote na  hatuwezi kuendelea kama vile tulivyo kuwa tukifanya kufikia sasa.

Kama viumbe hatuwezi kuishi bila uhusiano

Na akizungumzia juu ya maono ya viumbe duniani, Askofu Mkuu Paglia anasema, tunapotazama maisha yetu, dunia yetu maana ya siku nzima zetu, tunapaswa kuzingatia kuwa sisi sote tuna uhusiano wa mmoja na mwingine. Kila tendo la mtu mmoja haliwezi kuwa peke yake bali daima linategemea wengine na kwa ajili ya wema na mabaya. Na ndiyo maana kila uchaguzi, kama vile sera za kisiasa, kiuchumi, kijamii na binafsi, ikiwa havizingatii maono ya ulimwengu  kwa ajili ya wema wa pamoja au ubora wa kidugu, ni tishio la  kusababisha madhara makubwa.  Udugu  ni neno ambalo anaamini  Askofu mkuu Paglia kuwa linapaswa kuhusisha chaguzi zetu zote.

Sababu ya janga kwa mujibu wa maoni ya wengi ni kupuuzwa kwa hali ya hewa

Ushirikiano kati ya watu, ndani ya hali halisi ya miji, uhusiano kati ya mwanadamu na uumbaji, udugu kama ufikiaji wa umilele wa wote. Kutimiza elimu viumbe  ya ulimwengu ni kama kurudisha ndoto ya Mungu tangu mwanzo wa uumbaji. Uumbaji wote ni nyumba ya pamoja ya watu. Ushirikiano wa wanaume na wanawake lazima uwajibishe vizazi vyote na lazima uwajibishe kwa utunzaji wa nyumba hii amesisitiza.Yote haya yamepuuzwa. Sababu moja ya janga ni na  kwa mujibu wa walio nwengi, Askofu Mkuu amebainisha kuwa ni uharibifu wa hali ya hewa. Vifo vya wazee nchini katika vituo vya kutunzia wazee ni moja wapo ya matokeo ya uharibifu wa uhusiano kati ya vizazi. Tumeongeza maisha yetu,  anasema, ambayo ni bora, lakini baadaye tumewaweka wale tuli topewa zawadi hizi katika sehemu za mwisho wa maisha, kwa njia fulani tukiongezea ukatili huo.

Nafasi kubwa ya kiroho kupitia zaburi

Katika kitabu hicho ametoa nafasi kubwa hata kwa namna ya kusema ya uponyaji kiroho akitafakari zaburi ya 13, 22, 130 na  143, kwa sababu anaamini kwamba ni kipindi cha udhaifu mkubwa sana ambapo unaweza kuwakilisha na sura ya kile kilichotokea kwa Yesu juu ya Msalaba akiomba msaada. Aidha amesema kilio hicho pia kimeonyeswa na Papa Francisko tarehe 27 Machi 2020 katika uwanja mtupu wa Mtakatifu Petro akiwakilisha kilio cha binadamu kwa Mungu. Katika maana hiyo, utamaduni wa Kiyahudi-Kikristo umetuachia urithi wa kuomba kwa namna ya pekee katika kipindi cha majaribu makubwa. Na ndiyo maana anasema alipendelea kutazama tafakari hizo katika zaburi nne kwa sababu dunia nzima inahitaji sana. Kadhalika ameelezea juu ya kuguswa sana sala ya Papa ilivyoonyeshwa katika vyombo vya habari Ijumaa jioni na tendo lilotazamwa na mamilioni na milioni ya waitaliani ambao kwa hakika walikuwa ni waamini katoliki na wasio kuwa katoliki.

Zaburi zinakusanya hofu,mateso,kilio na matumaini

Kitabu cha Zaburi, pamoja na maombezi yake kwa Mungu, kinaweza kuwa alama muhimu kwa sababu kinakusanya hofu zetu, mateso yetu, kilio chetu, matumaini yetu, huzuni zetu. Aidha amebainisha ni jinsi gani alivyobaki amevutiwa siku zote  na rafiki yake mpendwa Elio Toaff, Mkuu wa wayahudi Roma. Yeye alikuwa akimwambia kuwa tangu akiwa kijana baba yake alikuwa anashauri achukue Kitabu cha Zaburi kila wakati. Baba yake alikuwa amemfafanulia ni jinsi gani ndani ya kitabu cha Zaburi yamo maisha yote  ya binadamu na Zaburi husaidia kukabiliana nayo. Aidha Toaff alikuwa akimsimulia kwamba wakati alipokuwa ametekwa na karibu kupigwa risasi, aliomba walinzi kabla ya kufa aweze kusali zaburi. Alijiweka kandoni ili kuomba na kimiujiza mmoja wa askari alimwambia atoroke. Kufuatia na tukio hilo lilimfanya awe na ibada kuu katika dini yake kwa kina na imani kwamba Mungu anakusaidia sana katika maisha. Lakini  Askofu Mkuu Paglia kwa kumalizia amesema kwamba anaamini Kitabu cha Zaburi wakati huu kinaweza kuwa alama ya kushangaza hata kwa wale ambao hawaamini.

29 April 2020, 17:39