Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Msaidizi Lambert Bainomugisha kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mbarara, Uganda. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Msaidizi Lambert Bainomugisha kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mbarara, Uganda. 

Askofu L. Bainomugisha, ateuliwa kuwa Askofu mkuu, Mbarara

Askofu mkuu mteule Lambert Bainomugisha alizaliwa tarehe 12 Julai 1961 huko Kashumba, Uganda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 13 Julai 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 2 Julai 2005, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Mbarara, Uganda na kuwekwa wakfu kuwa Askofu, tarehe 1 Oktoba 2005.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa na Askofu mkuu Paul Kamuza Bakyenga wa Jimbo kuu la Mbarara, Uganda. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Msaidizi Lambert Bainomugisha wa Jimbo kuu la Mbarara, kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mbarara, Uganda. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Lambert Bainomugisha alizaliwa tarehe 12 Julai 1961 huko Kashumba, Uganda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 13 Julai 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tarehe 2 Julai 2005, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Mbarara, Uganda na kuwekwa wakfu tarehe 1 Oktoba 2005 na Askofu mkuu Paul Kamuza Bakyenga wa Jimbo kuu la Mbarara. Tarehe 13 Novemba 2009 aliteuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Msimamizi wa Kitume “Sede plena et ad nutum Sanctae Sedis” wa Jimbo Katoliki la Hoima, lililokuwa wazi kuanzia tarehe 8 Februari 2014. Ametekeleza utume huu hadi tarehe 29 Februari 2016.

Jimbo Kuu la Mbarara, Uganda
25 April 2020, 14:34