Tafuta

Patriaki Barthlomew I, wa kiekume ametuma ujumbe wake kwa Papa Francisko na Rais wa Jamhuri ya Italia kuonesha ukaribu na mshikamano katika kipinid hiki cha janga la virusi Patriaki Barthlomew I, wa kiekume ametuma ujumbe wake kwa Papa Francisko na Rais wa Jamhuri ya Italia kuonesha ukaribu na mshikamano katika kipinid hiki cha janga la virusi 

Ujumbe wa Patriaki kwa Papa na Rais wa Italia

Patriaki Barthlomew I, wa kiekume ametuma ujumbe wake kwa Papa Francisko na Rais wa Jamhuri ya Italia kuonesha ukaribu na mshikamano katika kipinid hiki cha janga la virusi

Kwa mujibu wa Msemaji mkuu wa vyombo vya habari Vatican amethibitisha kuwa Patriaki wa kiekumene Bartholomew I amemtumia ujumbe Papa Francisko na Rais wa Jamhuri ya Nchi ya Italia Bwana Sergio Mattarella, katika kuonesha mshikamano wake kwa watu wa Italia kufuatia na janga hili la virusi vya corona.

Katika maandishi ya Patriaki huyo yanasisitizia roho ya sadaka na ujasiri uliooneshwa na watu wote, wahudumu wa Afya pia kutoa shukrani kwa jitihada za madaktari, wauguzi na watu wote wa kujitolea wanaoendelea kusaidia wagonjwa.

Na wakati huo huo, anaonesha hata ukaribu wake kwa wanafamilia wote waliopoteza wapendwa wao. Aidha Patriaki  Bartholomew I anawahakikishia maombi yake ya kila siku katika kipindi chote hiki cha kwaresima kwa wale wote ambao wamepoteza maisha, kwa ajili ya familia na ndugu wote.

23 March 2020, 15:27