Tafuta

Vatican News
TAHARIRI TAHARIRI 

Papa Francisko akiwa peke yake katika uwanja na Msalaba uliojaa machozi ya mbingu!

Picha,ishara na sala kwa ajili ya ulimwengu ambayo Papa Francisko amependelea kuadhimisha siku hii katika kuomba Mungu mwenyezi ili janga liishe.

ANDREA TORNIELLI

Mhusika mkuu wa sala ambaye jioni ya tarehe 27 Machi alikuwa katika Siku ya Ijumaa wakati Papa Francis ameadhimisha  kwenye uwanja ukiwa mtupu wa Mtakatifu Petro na kudumbukia kwenye ukimya usio wa kawaida, alikuwa ni Yeye, Yesu juu ya Msalaba! Msalaba na mvua iliyokuwa ikinyesha, maji yalichuruzikia mwili na kuweza kuifikia ile damu iliyochorwa katika mti wa msalaba wakati yale maji yalikuwa kama yale maji yanayosimuliwa katika Injili kwamba yalikushuka katika jeraha zilizo sababishwa na kuchomwa na mkuki.

Msalaba wa Kristo aliye sulubishwa ni ule alionusurika dhidi ya moto, ni  msalaba ambao Warumi waliutumia kuubeba wakati wa maandamano dhidi ya pigo kuu la janga la wakati ule. Ni ule mti wa Kristo msulibiwa ambaye Mtakatifu Yohane Paulo II aliukumbatia wakati wa fursa ya kitubio cha Jubilei ya mwaka 2000. Msalaba huo ulikuwa ndiyo mhusika mkuu wa ukimya wa kina na katikati ya nafasi iliyokuwa wazi na tupu. Hata Maria, Salus populi Romani, ( Maria afya ya waroma) aliyezungukwa na kioo ambacho hakikuonesha macho vizuri kutokana na ukungu kwa sababu ya mvua iliyokuwa ikinyesha na kuonesha macho yake ya unyenyekevu mbele ya mwanaye aliye tundikwa juu ya msalaba kwa ajili ya wokovu wa ubinadamu.

Picha ya sala ya Papa

Papa Francisko alionekana kuwa mdogo sana akiwa ameinama na kuchechemea wakati anapanda ngazi kwa ugumu kidogo ili kuweza kutoa sala yake chini ya miguu ya msalaba. “Bwana wewe  huoni kuwa tunaangamia? Uchungu wa kipeo hiki tunacho kihisi cha janga, kinafunua wazi ule  mwathiriko wetu na kuacha kufunika ule uju juu au usalama wa kijujuu ambao tumeujenga katika ratiba zetu, katika mipango yetu na katika mazoea yetu na kuweka vipaumbele vyetu na sasa tuko ndani ya bahari iliyochafuka, "tunaomba uamke ee Bwana".

Hini za magari ya huduma ya afya zilikuwa ni moja ya mambo mengi ambayo kwa masaa kama haya yanavuka na kupitia katika vitongoji vyetu ili kusaidia watu walio na maambukizi mapya pamoja  na kengele zikilia wakati wa kutoa baraka ya Ekaristi Urbi et Orbi, na wakati Papa akiwa peke yake, alirudi tena kwenye kiwanja hiki kama jangwa na kulowanishwa na mvua akifuatilia ishara ya msalaba akiwa na monstranti. Kwa mara nyingine tena mhusika mkuu alikuwa ni yeye, Yesu ambaye alijinyenyekeza na kutaka awe chakula, ambaye leo hii anarudia kusema  "Kwa nini unaogopa? Je! Bado haman imani?i Msiogope!

28 March 2020, 11:46