Tafuta

Vatican News
Uwanja na Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro vimefungwa kwa ajili ya taadhari. Uwanja na Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro vimefungwa kwa ajili ya taadhari. 

Coronavirus:Kanisa Kuu na Uwanja wa Mtakatifu Petro vimefungwa!

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican anasema hatua mpya za kizuizi hadi tarehe 3 Aprili zilizopitishwa na Mji wa Vatican kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa COVID-19, ni katika kushirikiana na maamuzi ya hivi karibuni yaliyochukuliwa na serikali ya Italia.Zipo lama tahadhari sehemu zinazofikiwa au zilizofungwa kwa ajili ya huduma zingine.

VATICAN NEWS

Kwa kushirikiana na maamuzi ya hivi karibuni yaliyochukuliwa na serikali ya Italia iliyofikia au iliyofungwa ufikiaji wa huduma zingine kama tahadhari kwa kila ngazi, hata mji wa Vatican unafuata sheria hizo na kwa namna ya pekee tangu tarehe 10 Uwanja na Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro vimefungwa kwa mahujaji wote na watalii.

Kizuizi hadi tarehe 3 Aprili

Siyo shuguli zote zimefungwa kwa mujibu wa msemaji mkuu wa vyombo vya habari kwa mfano Duka la madawa na Supermaket vitabaki vimefunguliwa lakini ni kwa ajili ya wafanyakazi tu. Na wakati huo huo  tangu tarehe 10 Machi kwa ajili ya tahadhari, wamefunga hata Ofisi ya Posta ya Vatican iliyopo kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro na Duka la Vitabu Vatican; Huduma ya utoaji wa Picha kwa njia ya  Osservatore Romani, japokuwa itabaki huduma  wazi kwa njia ya kuagiza kupitia katika mtandao vile vile kufungwa hata duka la nguo. Bwalo la chakula kwa ajili ya wafanyakazi litafungwa kwa ajili ya watu wa nje kuanzia tarehe 11 Machi na wakati huo huo huduma ya utoaji wa chakula itakuwa kwa njia kupeleka moja katika chakula katika vitengo vya kazi husika mjini Vatican lakini kwa kutoa maombi.  Hadi sasa wanafuata sheria ya kizuizi hiki hadi tarehe 3 Aprili 2020 endapo hapatakuwapo na mabadiliko.

Tahadhari kwa makanisa yaliyofunguliwa

Kuhusiana na tukio la uthibiti wa kueneza kwa virusi vya Corona, Makanisa katoliki  kwa duniani kote kwa namna moja au nyingine wamekwisha badili utaratibu wa ibada zao ikiwa ni jitihada za kuzuia maambukizi. Mapadre sasa wanawapa waumini ekaristi takatifu katika mikono badala ya ulimi na wameacha kutoa divai na kuwa na dawa ya kuzuia maambukizi mlangoni katika sehemu ya kuchovya maji ya baraka(senitizer). Badala ya kupeana mikono kama ishara ya amani, waamini wanaambiwa kumuombea jirani yake. Kesi hii ni ya aina yake na makanisa duniani kote wanapaswa kuchukua hatua thabiti kwa namna gani wanaweza kufanya kazi na serikali ili kuzuia maambukizi.

10 March 2020, 16:37