Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Miroslaw Adamczyk kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Argentina. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Miroslaw Adamczyk kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Argentina. 

Askofu mkuu Miroslaw Adamczyk, Balozi mpya wa Vatican, Argentina

Askofu mkuu Mirosław Adamczyk alizaliwa tarehe 16 Julai 1962 huko Gdańsk, nchini Poland. Baada ya majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 16 Mei 1987 alipewa Daraja takatifu ya Upadre. Tarehe 22 Februari 2013, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Gambia na baadaye Sierra Leone. Akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu tarehe 27 Aprili 2013.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Mirosław ADAMCZYK, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Argentina. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Adamczyk alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Panama. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Mirosław Adamczyk alizaliwa tarehe 16 Julai 1962 huko Gdańsk, nchini Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 16 Mei 1987 alipewa Daraja takatifu ya Upadre. Tarehe 22 Februari 2013, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Gambia na baadaye Sierra Leone. Akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu tarehe 27 Aprili 2013.

Tarehe 12 Agosti 2017, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Panama na akajisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya XXXIV ya Vijana Duniani huko Panama kuanzia tarehe 22 - 27 Januari 2019. Maadhimisho haya yaliongozwa na kauli mbiu “Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; iwe kwangu kama ulivyosema”. Lk. 1:38. Katika hija hii, vijana walisindikizwa kwa mfano, tunza na maombezi ya Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa kwa kutambua kwamba, Bikira Maria anaendelea kufanya hija pamoja na waamini kwa kuwaongoza vijana wa kizazi kipya, ili waweze kukita maisha yao katika imani, udugu na mapendo. Tarehe 22 Februari 2020 katika maadhimisho ya Siku kuu ya Ukulu wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Argentina!

Uteuzi Balozi Argentina

 

 

 

02 March 2020, 09:14