Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Joseph Mwongole kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Kitui nchini Kenya. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Joseph Mwongole kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Kitui nchini Kenya. 

Mh. Padre Joseph Mwongela ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Kitui, Kenya

Askofu mteule Joseph Mwongela alizaliwa tarehe 7 Aprili, 1968 huko Kakumi, Jimbo Katoliki la Kitui nchini Kenya. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 7 Septemba 1996 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baada ya hapo kama Padre alibahatika kuwa Paroko-usu, Paroko, Mlezi na Mkurugenzi wa Miito. Kunako mwaka 2008 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu kutoka Angelicum.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Joseph Mwongela wa Jimbo Katoliki la Kitui, Kenya, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kitui. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Joseph Mwongela alikuwa ni Makamu Askofu wa Jimbo Katoliki la Kitui. Askofu mteule Mwongela alizaliwa tarehe 7 Aprili, 1968 huko Kakumi, Jimbo Katoliki la Kitui. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 7 Septemba 1996 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baada ya hapo kama Padre alibahatika kuwa Paroko-usu, Paroko, Mlezi na Mkurugenzi wa Miito.

Kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2008 alitumwa na Jimbo kwenda Roma ili kujiendeleza kwa masomo ya juu, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian na kujipatia Shahada ya Uzamili na hatimaye, Shahada ya Uzamivu katika “Dogmatic Theology” kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thoma wa Akwino, maarufu kama Angelicum. Kipindi cha Mwaka 2008 alitoa huduma ya kichungaji kwenye Hospitali ya “Mater Misericordiae, Jimbo Katoliki la Kitui. Kati ya Mwaka 2008 hadi mwaka 2013 alikuwa ni Paroko wa Parokia ya Muthale, Jimbo Katoliki la Kitui. Kati ya Mwaka 2014-2015 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Yohane Paulo II kwa ajili ya masomo ya kitaaluma na Paroko wa Parokia ya Boma (Kanisa kuu la Our Lady of Africa). Na tangu mwaka 2015 hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kitui, amekuwa ni Makamu Askofu.

Askofu wa Jimbo la Kitui, Kenya

 

17 March 2020, 11:40