Tafuta

Papa Francisko atafanya ziara ya Kitume kisiwani Malta tarehe 31 Mei 2020. Mada ya ukarimu inaongoza ziara hii. Papa Francisko atafanya ziara ya Kitume kisiwani Malta tarehe 31 Mei 2020. Mada ya ukarimu inaongoza ziara hii. 

Ziara ya Kitume ya Papa huko Malta Mei 31!

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican tarehe 10 Februari 2020 imetangazwa ziara ya kitume ya Papa Francisko ya kutembelea moyo wa Bahari ya Mediterrania.Katika nembo ya ziara ya Papa inaongozwa na ujumbe wa ukarimu.

Kwa kupokea mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Malta, viongozi wa Nchi na wa Kanisa katoliki wa kisiwa hicho, Papa Francisko anatarajia kutimiza ziara yake ya Kitume huko kisiwani Malta na Gozo, tarehe 31 Mei 2020. Uratibu wa safari ya kitume utatolewa kwa wakati wake.

Hata hivyo katika ngao ya ziara ya Papa inaonesha mikono inayoelekeza Msalaba unaochomoza kutoka kwenye Merikebu ambayo inayumbishwa na mawimbi makuu; Mikono inawakilisha ishara ya ukarimu wa wakristo kwa jirani na msaada kwa wale wote wenye shida, waliachwa pweke katika hatima mbaya.

Merikebu inawakilisha janga la kutisha katika simulizi la manusura ya Mtakatifu Paulo kwenye Kisiwa cha Malta ( Mdo 27,27-44) ukarimu unawakilisha watu wa Malta kwa Mtume Paulo na manusura wenzake(Mdo 28,1-10). Katika simulizi hii hivi karibuni imerudiwa katika Katekesi za Papa Francisko. Kauli mbiu ya ziara ya Papa Francisko ya zaiara ya kitume ni: “walituonyesha fadhili zisizo za kawaida (Mdo 28, 2).

Mapapa wawili wa kwanza waliotembelea Kisiwa cha Malta ni Mtakatifu Yohane Paulo II, kuanzia tarehe 25-27 Mei 1990 na Papa Benedikto XVI kuanzia tarehe 17-19 Aprili 2010.

10 February 2020, 12:52