Tafuta

Vatican News
Nembo ya ziara ya kitume ya Papa Francisko kisiwani Malta tarehe 31 Mei 2020 Nembo ya ziara ya kitume ya Papa Francisko kisiwani Malta tarehe 31 Mei 2020 

Ziara ya kitume ya Papa Francisko huko Malta tarehe 31 Mei 2020!

Kwa kupokea tangazo kuhusu ziara ya kitume ya Papa Francisko katika moyo wa bahari ya Mediterrania,ikiwa ni kwa mara ya nne Papa anatembelea kisiwa hicho, Askofu Mkuu Scicluna anawaalika waamini kuanzia sasa wasali ili ziara ya Papa uweze kuwatia moyo katika uinjilishaji mpya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika kisiwa  cha Mallta kina jumla ya wakazi  karibia 500,000, ambapo itakuwa ni ziara fupi ya siku moja katika Sikukuu ya Pentekoste, lakini pia hata kufika Gozi  moja ya kisiwa kidogo  kati ya  visiwa vidogo 21 vinayounda Kisiwa cha Malta. Ziara ya Papa inafuata baada ya kupokea mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Malta, viongozi wa Nchi na wa Kanisa Katoliki wa kisiwa hicho ambapo  Papa Francisko anatarajia kutimiza ziara yake ya Kitume huko kisiwani Malta na Gozo, tarehe 31 Mei 2020. Uratibu wa safari ya kitume utatolewa kwa wakati wake.

Alama zilizomo katika Ishara ya ngao:ukarimu 

Katika ngao ya ziara ya Papa inaonesha mikono inayoelekeza Msalaba unaochomoza kutoka kwenye Merikebu ambayo inayumbishwa na mawimbi makuu; Mikono iliyoelekezwa juu pamoja inawakilisha ishara ya ukarimu wa wakristo kwa jirani na msaada kwa wale wote wenye shida, walioachwa pweke katika hatima yao mbaya.

Merikebu inawakilisha janga la kutisha katika simulizi la manusura ya Mtakatifu Paulo kwenye Kisiwa cha Malta (Rej Mdo 27,27-44) ukarimu unawakilisha watu wa Malta kwa Mtume Paulo na manusura wenzake (Rej Mdo 28,1-10). Katika simulizi hii hivi karibuni imerudiwa katika Katekesi za Papa Francisko. Kauli mbiu ya ziara ya Kitume ya Papa Francisko ni: “walituonyesha fadhili zisizo za kawaida (Mdo 28, 2).

Ni ziara ya nne ya Papa katika kisiwa cha Malta

Mapapa wawili wa kwanza waliotembelea Kisiwa cha Malta ni Mtakatifu Yohane Paulo II, kuanzia tarehe 25-27 Mei 1990 na Papa Benedikto XVI kuanzia tarehe 17-19 Aprili 2010. Katika ziara yake ya mwisho huko Malta kunako 2001,  katika  nyayo za Mtakatifu Paulo, Mtakatu Yohane Paulo alimtangaza mwenye heri Padre Ġorġ Preca, Mtakatifu wa kwanza wa Malta katika historia ya ukatoliki; sista Adeodata Pisani, Mkuu wa Monasteri ya Mtakatifu Petro katika mji wa Medina; na  Nazju Falzon, ndugu mdogo mfransiskani aliyekuwa akihudumia wanajeshi wakati wa Vita vya  Crimea.

Askofu Mkuu Scicluna: ziara ya Papa ni kuwatia moyo katika uinjilishaji

Katika video moja iliyotengenezwa akiwa katika groto moja ambamo kiutamaduni inasadikika kuwa Mtume Paulo  ndimo alihubiri Injili kwa miezi mitatu wakati wa akiwa  Kisiwa hicho, Askofu Mkuu Scicluna  wa Jimbo Kuu  La Valletta  amewaalika waamini wote wa Kisiwa cha Malta kusali, ili ziara hii ya Papa iweze kuwatia moyo kwa ajili ya uinjilishaji mmpya.  Uwepo wa Papa, anasisitiza  ni fursa kwa ajili ya kupyaisha ubatizo wao wa asili na katika roho yao ya ukarimu.

Watu wa Mungu wa Malata pia  wanaalikwa kutoa maisha kwa ajili ya wengine na kufariji majeraha ambayo kidogo anabinisha yameanza kusahulika na kuwekwa ukingoni mwa kijamii, lakini kwa maana hii wanaweza kujipyaisha ili waweze kupokea wengine ambao wanabisha mlango wa kisiwa chao na kuomba msaada ili wapate kweli kutambuliwa hadhi yao na ubinadamu kidogo.

11 February 2020, 14:58