Tafuta

Vatican News
Kardinali  Michael Czerny, akiwa katika mahojiano kuhusu Wosia wa Kitume 'Querida Amazonia' baada ya Sinodi Kardinali Michael Czerny, akiwa katika mahojiano kuhusu Wosia wa Kitume 'Querida Amazonia' baada ya Sinodi 

Czerny:ni muhimu kupenda Amazonia na watu wake ili kuokoa sayari!

Kardinali Czerny Katibu Maalum wa Sinodi ya Amazonia,amewakilisha Wosia wa Kipapa baada ya Sinodi kwamba Papa alimaliza Wosia tangu mwezi Desemba 2019 na ambao sasa umetolewa tarehe 12 Februari.Kwa hakika katika Wosia huu unaonesha ndoto nne kubwa za Papa kwa ajili ya Kanda ya Amazonia lakini pia hata ya Kanisa la kimisionari kuelekea Amazonia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wosia wa Kitume Querida Amazonia wa Papa Francisko uliotolewa tarehe 12 Februari 2020 unabainisha juu ya hatima ya Amazonia inayotugusa sisi sote kwa sababu kila kitu kimeunganisha nayo na wokovu wa Kanda hiyo, kwa watu wote asilia ni msingi kwa ajili ya dunia nzima. Kwa maana hiyo Kardina Michael Czerny, Katibu Maalum wa Sinodi ya Amazonia ameelezea juu ya Wosia  wa Kitume wa Papa baada ya Sinodi kwamba ulikabidhiwa kwao mwishoni mwa mwezi Desemba 2019. Na siku zilizofuata, wosia huo kufanyiwa kazi ya kuusoma na kuandaliwa, kwa kutafsiriwa katika  lugha nyingine na hatimaye sasa umetangazwa.

Moyo wa Wosia huu ni upendo wa Papa kwa ajili ya Amazonia na matokeo ya upendo huo. Ni mapinduzi kwa namna ya pamoja katika kufikiri juu ya uhusiano kati ya utajiri na umaskini, kati ya maendeleo na ulinzi; kati ya utetezi wa mizizi ya utamaduni na ufunguzi wa mwingine. Papa Francisko anapendekeza kwetu sisi anasema ule mwangwi ambao ulisababisha kuitisha kazi hiyo ya Sinodi. Na amefanya hivyo chini ya mtindo wa 2ndoto kuu nne”. Papa Francisko anaota kwa ajili ya Amazonia jitihada za wote katika kulinda haki za masikini zaidi, watu asilia, watu walio wa mwisho.  Papa anaota Amazonia ambayo inahifadhi utajiri wa utamaduni. Ndoto yake ya kiekolojia  ni Amazonia ambayo inahifadhi maisha yake yakusangaza. Na hatimaye   Papa Fra ciskoa anaota jumuiya  ya Kikristo yenye uwezo kuzaliwa upya ndani ya Amazonia  na kujenga Kanisa moja lenye uso wa kiamazonia.

Aidha Kardinali pia  amebainisha juu ya kushangazwa sana jinsi ndani ya Wosia wa Kitume ulivyo tajwa kwa wingi mashairi na mapapa waliopita. Hata hivyo Kardinali akizungumzia kuhusiana na ndoto hizi za  Papa, kardinali  amependa kukumbusha maneno ambayo Papa akizungumza na vijana mjini Roma kunako tarehe 11 Agosti 2018 alisema “ ndoto ni muhimu. Zinazidua maono kuwa mapana, zinasaidia kukumbatia maono yake na kukuza matumaini kwa kila tendo la kila siku… Ndoto zinakuamsha, zinakupeleka mbali. Ni kama nyota angavu zaidi, zile zinzoelekeza kuwa safari ndefu kuelekea ubinadamu… Hata hivyo Biblia inatwambia kuwa ndoto kubwa ni zile zenye uwezo wa kuleta matunda”

Kwa kujibu swali la mwandishi, Kardinali kuhusiana na ndoto amesitiza kwamba, kutokana na mtazamo wa ndoto hizo na matarajio hayo kwa hakika ndiyo matarajio yaliyo mapana. Ndoto ni maelekezo ya mchakato wa safari ambayo ni ya kanisa lote linavytakiwa lijikita kuwa nayo. Uzito wake upo katika kutazama maono, na siyo kuweka mlolongo wa sheria. Hakuna tangaza la upendo wenye kwa na mtindo wa mkataba, au orodha. Katika sura ya kwanza ambayo imejikita katika ndoto ya kijamii, Papa Francisko anatazama kwa kiasi kikubwa juu ya kuraruliwa kwa mazingira ya Amazonia na hatari za hadhi ya kibinadamu kwa watu ambao tayari hata Papa Mstaafu Benedikto XVI walikuwakiwa amesha sema na kuwalika watazame suala hili.

Anasema kuwa lazima kikasirika kwa sababu siyo vizuri kuzoea mabaya. Anawaalika kujenga mitindo ya mshikamano na maendeleo ambayo yashinde tofauti mawazo na kasumba za ukoloni. Papa Francisko anawalika kutafuta mbadala wakufuga na kilimo endelevu, nguvu za nishati zisizo chafuzi, rasilimali za kufanya kazi ambazo hazipelekei uharibifu wa mazingira na tamaduni. Kwa ujumla ndoto kubwa hizi anasisitia Kardinali, zinahitaji kutosinzia lakini kujikita kwa dhati katika shughuli hizo na kila siku.

13 February 2020, 09:29