Tafuta

Biashara haramu ya binadamu ni udhalilishaji wa utu,heshima na haki msingi za binadamu ni jambo ambalo ni kinyume kabisa cha maadili na utu wema.Ni sala kwa ajili ya waathirika Biashara haramu ya binadamu ni udhalilishaji wa utu,heshima na haki msingi za binadamu ni jambo ambalo ni kinyume kabisa cha maadili na utu wema.Ni sala kwa ajili ya waathirika 

Tarehe 8 ni Siku kupinga biashara haramu ya watu duniani

Tarehe 8 Februari inaadhimiishwa siku ya VI duniani kwa ajili ya maombi na tafakari kuhusu Biashara ya binadamu na utumwa ambayo iliwekwa siku ya kumbu kumbu ya Mtakatifu Bakhita,mtawa mkanosiani mwenye asili ya Sudan ambaye amegeuka kuwa ishara duniani ya jitihada za Kanisa katika kupambana na biashara hiyo mbaya.Katika madhabahu ya Loreto sala ya rosari itafanyika saa 3.00 usiku majira ya Ulaya..

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wanawake, watoto wa kiume, kike na hata wanaume wote wanaweza kuwa waathirika wa biashara haramu ya watu, kutegemea na mambo kama  unyanyasaji wa kijinsia au kazi za suruba, ukahaba  mambao ambayo hajali umri na wala aina ya mtu. Biashara haramu ya binadamu ni undhalilishaji wa utu, heshima na haki msingi za binadamu ni jambo ambalo ni kinyume kabisa cha maadili na utu wema. Biashara haramu ya binadamu inaleta utajiri kwa  kundi la mafisadi na watu wanaotaka utajiri wa haraka haraka hata kama ni kwenda kinyume cha sheria na kanuni maadili. Kanisa limekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu kwa nyakati mbali mbali, kwani ni jambo ambalo linapingwa si tu katika maisha ya kiroho, bali hata katika tamaduni za watu kwani ni jambo ambalo linagusa utu na heshima ya binadamu.

Siku ya kupinga  Biashara ya binadamu na utumwa ambayo inaadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 Februari ya kila mwaka, sambamba na kumbukumbu ya liturujia  ya Mtakatifu Josephina Bakhita ambaye ni mwathirika wa utumwa. Duniani kuna milioni 40 ya watu ambao wanajikita katika hali hii ya kutisha na zaidi ni asilinia 70 ni wanawake na wakati huo karibia asilimia 20 ni watoto, ndiyo ni idadi, lakini kwa bahati mbaya ni zaidi. Janga hili limezidi kuongezeka zaidi hasa katika mantiki ya za kivita, uhamisha wa kulazimishwa na ambao hasa unaona ongezeka kwa watoto wengi wae wa kike na kiume. Talitha Kum, mtandao wa Kimataifa wa Mama wakuu wa Mashirika ya Kitawa dunianiwanaojikita katika shughuli za kuwasaidia waathirika, na ambapo katika ripoti yao ya mwaka 2018 waweze kuwasaidia karibu watu 15,000 ambao wameondokana na biashara hii katika sehemu mbali mbali za dunia.

Kufuatia na tukio la Siku ya kupinga biashara ya watu tarehe 8 Februari, katika Madhabahu ya Kimataifa ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Loreto watasali rosari kwa ajili ya kuombea waathirika  wa biashara na kwa ajili ya wagonjwa wote. Ni taarifa kutoka wawakilishi wa Papa ambapo sala ya Rosari na mishumaa tarehe 8 Februari  2020 kuanzia saa 3.00 usiku  majira ya Ulaya katika. Sala hiyo itaongozwa na Mwakilishi wa kitume Askofu Mkuu Fabio Dal Cin, katika fursa ya Siku ya Kupinga biashara ya utumwa wa watu sambamba na Sikukuu ya Mtakatifu Giuseppina Bakhita, watasali kwa ajili ya wahanga wa biashara hiyo, lakini pia katika matarajio ya Siku ya Wagonjwa duniani itakayoadhimisha tarehe 11 Februari , nia pia itakuwa kwa ajili ya wagonjwa wote.

07 February 2020, 15:37