Tafuta

Vatican News
Uwanja wa Mtakatifu Anselmi Roma Uwanja wa Mtakatifu Anselmi Roma   (Vatican Media)

Tarehe 26 Februari Papa ataadhimisha misa na kupaka Majivu!

Papa Francisko anatarajia kuadhimisha misa Takatifu katika Basilika ya Mtakatifu Sabinana wakati Mama Kanisa anaanza kipindi cha Kwaresima.Maandamano ya kuelekea katika Kanisa hilo yataanzia katika Basilika ya Mtakatifu Anselmi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Msemaji wa vyombo vya habari Vatican, ametoa ripoti rasmi ya ratiba ya shughuli ya Papa Francisko kwa siku ya tarehe 26 Februari 2020, siku ambayo ni mwanzo wa kipindi cha Kwaresima. Ukiwa katika Dari ya Tao ya Mtakatifu Petro unaona kwa mbali sana kati ya taa za aina tatu na taa za aina nne ambapo zinaonesha kengele za kirumi huko juu. Na hiyo ni Basilica ya Kibenedikitini ya Mtakatifu Anselmi ambayo kwa mara nyingine tena inajiandaa kukaribisha tukio la kuanza kwa kipindi cha  Kwaresima kwa mapapa ambapo kwa sasa ni miaka 48 tangu wakati Papa Roncalli aliyeanzisha utamaduni huo na kurithishwa tabia hiyo ya Zama za Kati hadi sasa.

Hii itafanyika tarehe 26 Machi siku ya majivu kwa kuanza na  liturujia ya maandamano itakayoanza saa 10.30 jioni  majira ya Ulaya  kutoka katika  Basilika ya Mtakatifu Anselmi yakiongozwa na Papa Francisko mwenyewe  na kwa  hatua za mita 300 hivi kufika katika Basilika ya Mtakatifu Sabina, ambapo nalo ni jiwe msingi wa Ukristo. Saaa 11.00 masaa ya Ulaya Papa Francisko ataongoza Misa Takatifu na kupaka majivu.

Aidha kwa mujibu wa utamaduni mwingine ambao kwa sasa unajulikana utakuwa ni siku ya Jumapili tarehe Mosi  Machi, Papa Francisko na wahudumu wengine katika Sekretarieti ya Vatican watapanda bus kuelekea Ariccia nje kidogo ya Roma katika mafungo ya kiroho hadi Ijumaa tarehe 6 Machi 2020.

19 February 2020, 17:03