Tafuta

Taasisi ya Kipapa ya Maisha kuanzia tarehe 26-28 Februari 2020 imeadhimisha Mkutano wake wa 26 kuhusu: Akili Bandia Taasisi ya Kipapa ya Maisha kuanzia tarehe 26-28 Februari 2020 imeadhimisha Mkutano wake wa 26 kuhusu: Akili Bandia 

Taasisi ya Kipapa ya Maisha: Mkutano 2020:Akili Bandia

Kuanzia tarehe 26 hadi tarehe 28 Februari 2020, Taasisi yake inaadhimisha Mkutano mkuu wa ishirini na sita unaojikita katika matumizi ya “artificial intelligence” yaani “akili bandia” kwa ajili ya huduma ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, hususan katika sekta ya afya. Mkutano huu unapania pamoja na mambo mengine kuchambua: kanuni maadili, haki msingi za binadamu na afya.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Kipapa ya maisha iliyoanzishwa tarehe 11 Februari 1994, anasema, kuanzia tarehe 26 hadi tarehe 28 Februari 2020, Taasisi yake inaadhimisha Mkutano mkuu wa ishirini na sita unaojikita katika matumizi ya “artificial intelligence” yaani “akili bandia” kwa ajili ya huduma ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, hususan katika sekta ya afya. Mkutano huu unapania pamoja na mambo mengine kuchambua: kanuni maadili, haki msingi za binadamu na afya.

Takwimu zinazonesha kwamba, kuna washiriki 356 kutoka katika nchi 41 wengi wao wakiwa ni vijana wa kizazi kipya. Mkutano huu unahudhuriwa na wasomi pamoja na viongozi wa ngazi ya juu kutoka katika Jumuiya ya Kimataifa, akiwemo Bwana Dongyu Qu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO pamoja na Bwana Brad Smith, Rais wa Kampuni ya Microsoft. Mkutano huu unaendeshwa kwa kuzingatia Mafundisho tanzu ya Kanisa kuhusu Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo; tunu msingi za maisha ya Kiinjili kuhusu zawadi ya maisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Haya ni mambo msingi yanayopewa kipaumbele cha kwanza na Taasisi ya Kipapa ya Maisha, ili kuibua na kuendeleza mang’amuzi na uzoefu wa maisha ya binadamu, ili kudumisha Injili ya uhai. Habari Njema ya Wokovu kuhusu maisha ya binadamu inawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujenga na kudumisha majadiliano katika ukweli na uwazi na wasomi pamoja na wanazuoni; wanasiasa na watetezi wa haki msingi za binadamu bila kuwasahau wale wote wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya kutetea na kudumisha Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo! Kimsingi mkutano huu mkuu umejikita zaidi katika kanuni maadili na utu wema.

Askofu Mkuu Paglia

 

28 February 2020, 15:11