Tafuta

Vatican News
Kwaresima ni Kipindi muafaka cha kutenga muda kwa ajili ya kusoma, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili. Kwaresima ni Kipindi muafaka cha kutenga muda kwa ajili ya kusoma, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili.  (Vatican Media)

Kwaresima ni kipindi cha kufunga Luninga na Simu za viganjani!

Kwaresima ni kipindi muafaka cha kutenga muda kwa ajili ya kusoma, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika matendo ya huruma. Ni kipindi cha kuzima luninga na kufungua Biblia tayari kusoma Neno la Mungu ambalo ni taa na dira ya maisha. Baba Mtakatifu anakaza kusema, Kwaresima ni wakati uliokubaliwa wa kujibandua na matumizi ya simu za mkononi, ili kujiunga na Injili!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii anasema, Kwaresima ni kipindi muafaka cha kutenga muda kwa ajili ya kusoma, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili. Ni kipindi cha kuzima luninga na kufungua Biblia tayari kusoma Neno la Mungu ambalo ni taa na dira ya maisha. Baba Mtakatifu anakaza kusema, Kwaresima ni wakati uliokubaliwa wa kujibandua na matumizi ya simu za viganjani, ili kujiunga na Injili! Huu ni ushauri wa Baba Mtakatifu unaopani kuwawezesha waamini na watu wote wenye mapenzi mema kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya maadhimisho ya Fumbo la Pasaka, kiini cha imani ya Kikristo!

Wakati huo huo, Dr. Matteo Bruni Msemaji mkuu wa Vatican katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amebainisha kwamba, Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 28 Februari 2020 ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatican. Kutokana na sababu zilizoko nje ya uwezo wake, shughuli nyingine zote zilizokuwa zimepangwa kwenye ratiba ya Ijumaa, tarehe 28 Februari 2020 zimefutwa, ili kumpatia fursa ya kuendelea kuimarisha afya yake, ambayo kwa siku za hivi karibuni ilidhohofu kidogo!

Dr. BRUNI: Taarifa II.

 

28 February 2020, 14:34