Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake, ameshindwa kuhudhuria Ibada ya toba na upatanosho kwa wakleri wa Jimbo kuu la Roma, 27 Februari 2020. Baba Mtakatifu Francisko kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake, ameshindwa kuhudhuria Ibada ya toba na upatanosho kwa wakleri wa Jimbo kuu la Roma, 27 Februari 2020.  (Vatican Media)

Ibada ya toba na upatanisho kwa wakleri wa Jimbo kuu la Roma 2020

Kadiri ya ratiba elekezi, Baba Mtakatifu Francisko alikuwa anatarajiwa kwenda kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane wa Lateran kwa ajili ya kuadhimisha Liturujia ya Toba kwa Wakleri wa Jimbo kuu la Roma. Dr. Bruni anasema, lakini kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, Baba Mtakatifu ameshindwa kuhudhuria Ibada hii na badala yake, ameendelea na utume wake mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Dr. Matteo Bruni Msemaji mkuu wa Vatican katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amebainisha kwamba, Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 27 Februari 2020 ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatican. Kadiri ya ratiba elekezi, Baba Mtakatifu alikuwa anatarajiwa kwenda kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane wa Lateran kwa ajili ya kuadhimisha Liturujia ya Toba kwa Wakleri wa Jimbo kuu la Roma. Dr. Bruni anasema, lakini kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, Baba Mtakatifu Francisko ameshindwa kuhudhuria Ibada hii na badala yake, ameendelea kutekeleza dhamana na wajibu wake wa kawaida katika makazi yake ya Mtakatifu Martha, hapa Vatican.

Shughuli nyinginezo zimeendelea kama kawaida! Ratiba elekezi inabainisha kwamba, Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 27 Februari 2020 angeongoza Ibada ya Upatanisho, mwanzoni mwa Kipindi cha Kwaresima kwa wakleri wa Jimbo kuu la Roma. Na Kardinali Angelo De Donatis, Makamu wa Askofu Jimbo kuu la Roma angetoa tafakari na baada ya hapo, wakleri wangeingia kwenye “Mahakama ya toba na huruma ya Mungu” kwa kuungama dhambi zao. Kama kawaida, Baba Mtakatifu angetumia fursa hii pia kujipatanisha na Mungu na baadaye, kuwaungamisha wakleri kadhaa.

Dr. Bruni
27 February 2020, 14:27