Tafuta

Vatican News
Papa amekutana na Rai wa Jamhuri ya Hungary Bwana Janos Ader visits Vatican Papa amekutana na Rai wa Jamhuri ya Hungary Bwana Janos Ader visits Vatican  (AFP)

Papa Francisko amekutana na Rais wa Hungary,Bwana János Áder

Katika mazungumzo ya Rais wa Hungary na Katibu wa Vatican ni pamoja na kuonesha mahusiano mema yaliyopo baina na nchi hizo mbili na Madhimisho ya 52 ya Kongamano la Kimataifa la Ekaristi Takatifu huko Budapest kunako Septemba 2021.Mada nyingine zilizoguswa ni kuhusu haki kijamii,ukarimu,uhamasishaji wa familia,utunzaji wa mazingira,wakati uliopo na ujao kwa ajili ya Ulaya.

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican amethibitisha kuwa Alhamisi tarehe 14 Februari 2020, Papa Francisko amekutana na Rais János Áder, wa Jamhuri ya nchi ya Hungary, ambapo mara baada ya mkutano huo pia amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akisindikizwa na monsinyo Miroslaw Wachowski, Katibu msaidizi wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na nchi za nje.

Katika mazungumzo yake na Katibu wa Vatican, yameonesha uwepo wa mahusiano mema baina na nchi zote mbili na pia kuzungumzia maadhimisho ya mwaka wa 30 tangu kuwa na mkataba…aidha kwa namna ya pekee  wamegusia kuhusu  maadhimisho ya Kongamano la 52 la Ekaristi  Tafaktifu kitaifa huko  Budapest Septemba 202.

Mada nyingine walizogusia ni kuhusu haki kijamii, ukarimu, uhamasishaji wa familia, utunzaji wa mazingira, wakati uliopo na wakati endelevu wa bara la  Ulaya.

14 February 2020, 15:44