Tafuta

Mkutano wa Makardinali washauri wa Papa Mkutano wa Makardinali washauri wa Papa  

Papa Francisko na C6,siku tatu za kukabiliana!

Tarehe 17 Februari mjini Vatican umefunguliwa Baraza la makardinali washauri wa Papa akiwepo hata yeye na utahtiimishwa siku ya Jumatano.Ni mwendelezo wa mafunzo kuhusu mchakato wa Katiba Mpya ya Kitume

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Makardinali wa washauri wa Papa wamerudia kukutana na Papa Francisko ikiwa ni mkutano wa 33 wa Baraza la Makardinali  washauri. Kama kawaida ya Mkutano wao utajikita kwa siku tatu kuanzia 17 hadi 19 Februari 2020. Katika meza yao  wanaendeleza rasimu ya hati ambayo itabadilisha ile ya “Pastor Bonus”, ya katiba ya Kitume iliyotangzwa na Mtakatifu Yohane Paulo II na kuanza kufanya kazi yake tarehe 28 Juni 1988, , ambayo inajumuisha vifungu 193, Adnexum 2 na ambayo baadaye ilifanyiwa marekebisho yaliyoletwa na Papa Mstaafu Benedict XVI na Papa Francisko.

Kazi zilizotangulia

Kati ya tarehe 2 na 4 Desemba 2019 ilikuwa ni mkutano wa 32 wa Baraza la makardinali washauri wa Papa ambao walendelea wakiwa na Papa kwa kukabiliana na rasimu hiyo mpya ya Katiba ya kitume. Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari wanasema umakini ulikuwa umewekwa  kuhusu uhusiano kati ya Vatican na Mabaraza ya Maaskofu na kuhusu uwepo wa waamini walei kwa wanaume na wanakwa , katika maamuzi ya nafasi kwenye ofisi za Kapapa  hata katika mashirika mengine ya Kanisa na kufanya utafiti katika misingi ya Kitaalimungu -Kichungaji kuhusiana na mantiki hizi.

Mapendekezo ya tafiti

Kwa mujibu wa vyombo vya habari Vatican, pia katika meza ya Baraza la Makardinali washauri ilikuwa imefikia baadhi ya mapendekezo ya Katiba moja ya kutume kuhusiana na ukusanyaji   wa zana hadi siku chache kabla ya mkutano wa sasa, ambapo shughuli ya kutathimini, ingeendelea kwa mujibu wa habari za mwezi Desemba na katika sehemu ya mkutano wa mwezi Februari 2020.

17 February 2020, 16:52