Tafuta

Vatican News
Papa Mstaafu hajatoa idhini ya mpango wowote wa kitabu kilichosaniwa na wote wawili,kuhusu Useja wa kikuhani kinachotarajiwa kutolewa tarehe 15 Januari 2020 nchini Ufaransa.  Papa Mstaafu hajatoa idhini ya mpango wowote wa kitabu kilichosaniwa na wote wawili,kuhusu Useja wa kikuhani kinachotarajiwa kutolewa tarehe 15 Januari 2020 nchini Ufaransa.  

Uthibitisho wa kitabu kuhusu useja kwa mujibu wa Ask.Mkuu Gänswein!

Rais wa nyumba ya Kipapa na Katibu maalum wa Papa mstaafu amethibitisha kuwa Papa Benedikto XVI hakutoa ruhusa ya kuweka sahini mbili kama inavyoonesha katika kitabu.

VATICAN

Askofu Mkuu Georg Gänswein, Rais wa nyumba ya Kipapa na Katibu maalum wa Papa mstaafu ameacha uthibitisho katika Shirika la Kna na Ansa kuhusiana na kitabu juu ya useja ambacho kitatolewa tarehe 15 Januari 2020 nchini Ufaransa kikiwa na sahini ya Papa Benedikto XVI na Kardinali  Robert Sarah.

Ninaweza kuthibitisha kwamba leo asubuhi katika maelekezo ya Papa Mstaafu, nimemwomba Kardinali Robert Sarah awasiliane na waariri wa kitabu akiomba waondoe jina la Benedikto XVI kama mwandishi mwenza wa kitabu hicho na kuondoa sahini yake hata katika utangulizi na  katika hitimisho la kitabu hicho”.

 “Papa Mstaafu kwa hakika alikuwa anajua kuwa Kardinali alikuwa anaandika kitabu, ameongeza - Gänswein  na alikuwa amemtumia maandishi yake mafupi kuhusu ukuhani na kumruhusu aweze kuyatumia kama anavyotaka. Lakini hakuwa ametoa idhini ya mpango wowote wa  kitabu kilichosaniwa na wote wawili,  wala hakuwa amekiona kuidhinisha jalada la kitabu. Hii imetokana na kutokuelewana, bila kuweka mashaka ya nia njema ya Kardinali Sarah.

14 January 2020, 13:13