Tafuta

Vatican News
Waamini wote mnaalikwa kuungana na Papa Francisko katika kusali Rosari kwa ajili ya kuombea amani duniani Jumamosi tarehe 11 Januari 2020,saa tatu kamili usiku majira ya Ulaya. Waamini wote mnaalikwa kuungana na Papa Francisko katika kusali Rosari kwa ajili ya kuombea amani duniani Jumamosi tarehe 11 Januari 2020,saa tatu kamili usiku majira ya Ulaya. 

Tarehe 11 Januari saa 3.00 usiku tunaombwa kusali Rosari na Papa Francisko!

Waamini wote duniani wanaalikwa kuungana na Papa Francisko kusali Rosari Takatifu kwa ajili ya kuombea amani na historia ya dunia ya leo.Sala ya Rosari Takatifu itaongozwa na Askofu Mkuu Fabio Dal Cin Mwakilishi wa Kipapa katika madhabahu ya Mama Yetu wa Loreto,Jumamosi tarehe 11 Januari 2020,saa 3.00 usiku majira ya Ulaya.

Uwakilishi wa Kipapa unatoa taarifa kuwa, nia ya Papa ya kusali Rosari na mishumaa kunako tarehe 11 Januari 2020 saa 3,00 majira ya Ulaya, itafafanyika katika Madhabahu ya Mama Maria wa Loreto na abaadaye kufuatia maandamano katiak Uwanja wa Mama, kwa kuongozwa na Askofu Mkuu Fabio Dal Cin Mwakilishi wa Kipapa katika Madhabau hiyo na ambaye atakuwa ameungana na Papa Francisko kusali kwa ajili ya amani dunianai na kwa ajili ya umoja wa Wakristo na wale wote wanaoteseka na kusongwa.

Ikumbukwe Papa Francisko wakati wa tafakari ya katekesi kwa waamini na mahujaji, wiki hii akikumbuka manusura ya Paulo  na wenzake kwa mujibu wa Maandiko katika Kitabu cha Matendo ya Mitume, Papa alibainisha juu ya majanga yaliyo wakumba hadi kunusurika kwa Paulo na kundi lake. Manusuru hao walifika  katika kisiwa cha Malta mahali ambapo wakazi walionesha ukarimu na kuwapokea. Aliwapongeza Papa watu wa kisiwa hicho kwa ukarimu. 

Na mwisho wa katekesi yake, Papa Francisko aliwaalika watu wawe makini kwa manusura wengi wa historia ya sasa na ambao wanafika katika miambao yetu na ili hata sisi tuweze kuwapokea kwa ule upendo wa kidugu ambao unatokana na kukutana na Yesu. Na hiyo inaokoa ubaridi wa sintofahamu na hukosefu wa ubinadamu. kwa kufuata mfano wa ukarimu huo tunaalikwa sote  kuungana na Papa Francisko ili kusali kwa ajili ya amani duniani na kwa ajili ya mateso ya wakristo wengi katika historia ya dunia .

10 January 2020, 15:09