Tafuta

Vatican News
2018.07.07 Visita a Bari Incontro di Preghiera CPF 2018.07.07 Visita a Bari Incontro di Preghiera CPF  (Vatican Media)

Ratiba elekezi ya maadhimisho ya Papa mwezi Januari na Februari!

Tarehe 23 Februari Papa Francisko anatarajia kuadhimisha Misa Takatifu huko Bari, Italia katika Mkutano kuhusu“amani katika Mediterranea,kwa mujibu wa ratiba elekezi ya maadhimisho ya kiliturujia ya Papa katika mwezi wa Januari na Feberuari 2020,iliyotolewa tarehe 7 Januari.

Tangu maadhimisho ya masifu ya jioni kwa ajili ya Siku ya 53 ya  Kuombe Umoja wa Wakristo, arehe 25 Januari saa 11.30 masaa ya Ulaya, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta, ikiwa ni fursa ya Sikukuu ya Uongofu wa Mtu PauloPaulo, hadi kufikia Misa itakayo fanyika huko Bari tarehe 23 Februari 2020, kwenye Mkutano kuhusu Tafakari na Tasaufi ya “Mediterrranea mpaka wa amani”. Ndiyo yanayo onekana katika kipindi cha maadhimisho ya Liturujia za Papa Francisko kwa mwezi Januari na Februari 2020 kwa mujibu wa ratiba elekezi iliyotolewa na vyombo vya habari Vatican, tarehe 7 Januari 2020.

Dominika tarehe 26 Januari 2020, Papa Francisko anatarajia kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika fursa ya “Dominika ya Neno la Mungu” katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,na wakati huo huo Jumamosi ya kwanza ya mwezi Februari, katika katika fursa ya maadhimisho ya Siku kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni sanjari na maadhimisho ya Siku ya XXIV ya Watawa Duniani, saa 11.00 jioni majira ya Ulaya, Papa Francisko anatarajia kuongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa wajumbe wa Mashirika ya Kitawa na vyama vya kitume na waamini wenye mapenzi mema katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

07 January 2020, 14:23