Tafuta

Vatican News
Tarehe 31 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na Rais wa Jumhuri ya Argentina,Bwana Alberto Fernández Tarehe 31 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na Rais wa Jumhuri ya Argentina,Bwana Alberto Fernández  

Papa Francisko amekutana na Rais wa Argentina Bwana Alberto Fernández

Tarehe 31 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na Rais wa Jumhuri ya Argentina,Bwana Alberto Fernández na ambaye baada ya mkutano huo amekutana na Kardinali Pietro Parolin, katibu wa Vatican akisindikizwa na monsinyo Mirosław Wachowski,katibu msadizi wa Vatican wa mahusiano na ushirikiano na nchi za nje.

VATICAN

Kwa mujibu wa Msemaji wa vyombo vya habari Vatican Dk. Bruni amethibtisha kuwa katika Jumba la kitume asubuhi tarehe 31 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na Rais wa Jumhuri ya Argentina, Bwana Alberto Fernández na ambaye baada ya mkutano huo amekutana na Kardinali  Pietro Parolin, katibu wa Vatican akisindikizwa na monsinyo Mirosław Wachowski, katibu msadizi wa Vatican wa mahusiano na ushirikiano na nchi za nje.

Katika mazungumzo na viongozi wao wameelezea juu ya mahusiano mema kati ya Vatican na Jamhuri ya Argentina. Pia kugusaia hali halisi ya nchi hasa kwa baadhi ya matatizo kama vile kipeo cha uchumi mapambano dhidi ya umaskini, rushwa na biashara haramu ya madawa , huamasishwaji kijamii, na kulinda maisha tangu kutungwa kwake hadi kifo chake, mada ambayo imezungumzwa kwa viongozi hawa na si kwa Papa.

Katika mantiki hiyo pia wameonesha mchango mkubwa unaotolewa na  Kanisa Katoliki katika jumuiya nzima ya jamii ya nchi ya Argentina hasa katika sehemu ya watu walioathirika zaidi. Vile vile wamegusia hata masuala ya pamoja katika mantiki ya kikanda.

31 January 2020, 14:40