Tafuta

Vatican News
Mamandamano ni makubwa sana nchini Iran kufuatia na kifo cha Suleimani aliyekuwa kiongozi maarufu katika nchi hiyo Mamandamano ni makubwa sana nchini Iran kufuatia na kifo cha Suleimani aliyekuwa kiongozi maarufu katika nchi hiyo  (ANSA)

Papa anafuatilia kwa wasiwasi juu ya mgogoro kati ya Marekani na Iran

Askofu Mkuu Leo Boccardi Balozi wa kitume Jijini Teharan kwa njia ya simu ameelezea kuhusu hali halisi ya mivutano iliyopo na maandamano makubwa kufuatia na kuuwawa kwa Jenerali Sulemaini baada ya mashambulizi ya Waamerika na kwa maana hiyo anasisitiza kwamba inahitajika silaha za majadiliano na haki lazima itumike

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuongezeka kwa mzozo kati ya Washington na Teheran, kufuatia na kifo cha mmoja wa watu muhimu aliyeanzisha uwepo wa msimamamo wa wairan  Jenerali Qassem Soleimani, ambaye alishambuliwa na shambulio la anga la waamerika, unaamsha hata  mshtuko katika mji wa Vatican na Papa Francisko ambaye anafuatilia mwendelezo wa hali halisi hiyo anasali kwa ajili ya amani. Ndiyo mawazo ambayo amesema Balozi wa Vatican wa Kitume katika nchi ya Iran, Askofu Mkuu Leo Boccardi, wakati akihojiana kwa njia ya simu na Vatican News.

Papa amearifiwa juu ya kile kinachoendelea kutokea katika masaa yote hayo katika mkoa mzima na pia nchini Iran, baada ya kuuawa kwa Jenerali Solemaini. Hii yote inaleta wasiwasi na inaonyesha jinsi gani ilivyo  ngumu kujenga na kuamini amani. Siasa nzuri iko kwenye huduma ya amani, jamii nzima ya kimataifa lazima ijiweke katika huduma ya amani, siyo tu katika kanda hiyo bali katika ulimwengu wote. Hakika, katika masaa hayo alisema, kuna mvutano mkali nchini Iran. Kumekuwa na maandamano ambapo baada ya kuthibitisha ukweli vimetokea vurugu huzunu na maandamano makubwa, amesema.

Katika wakati huu mgumu sana na dhaifu sana, jambo la kufanya anasema ni wito mku wa kupunguza mvutano uliopo na hasa kuwaalikwa wote katika mchakato wa mazungumzo na kuamizi katika majadiliano kwani historia imekuwa ikitufundisha kila wakati, kwamba vita na silaha sio suluhisho la shida zinazoikabili ulimwengu wa leo. Mazungumzo lazima yaamini. Lazima tuamini katika mazungumzo. “ Ni lazima  kuamini katika mchakato; Pia ni lazima kuamini majadiliano. Na lazima kuacha mizozo na kujipanga kwa silaha zingine tofauti ambazo ni za haki na kuwa nia njema.

Hata hivyo ili kuweza kutumia njia hii nyingine ya silaha za haki na nia njema  anashauri awali ya yote kuwa inahitaji  kuendelea kkukazia na kuwamba  kuwa  na makini katika Jumuiya ya kimataifa kuhusu hali ya nchi za Mashariki. Hali katika nchi za Mashariki ya Kati, lazima iendelezwe kupata suluhisho na kuwahimiza wote wahusika kuhusu jukumu moja kwa moja ambalo tunalo. “Pacta sunt servanda”, inasema sheria muhimu ya diplomasia, anaongeza. Na kanuni  za sheria lazima ziheshimiwe na kila mtu.

04 January 2020, 13:39