Tafuta

Tarehe 26 Januari 2020 Papa amemchagua Gonzalo Aemilius kuwa katibu wake maalum Tarehe 26 Januari 2020 Papa amemchagua Gonzalo Aemilius kuwa katibu wake maalum 

Padre Aemilius ni katibu mpya maalum wa Papa!

Padre wa Urguay ambaye Papa Francisko amemfahamu tangia 2006 anachukua nafasi ya katibu maalum iliyoachwa na Padre Pedacchio mwezi Desemba 2019

VATICAN NEWS

Padre Gonzalo Aemilius anajuana na Papa Francisko tangu 2006 wakati Papa bado akiwa ni Askofu Mkuu wa Buenos Aires ambapo alimpigia simu kwa maana alikuwa amesikia sifa zake kuhusu kazi aliyokuwa anaitenda ya vijana wa barabarani. Padre Gonzalo Aemilius,  wa Uruguay ana shahada ya udaktari wa taalimungu ambaye amechaguliwa kuwa Katibu Maalum wa Papa Francisko. Yeye anachukua nafasi iliyoachwa na Padre Fabian Pedacchio, kutoka Argentina ambaye amekuwa na Papa Francisko tangu 2013 hadi 2019, baada ya kurudi kwao nchini mwezi Desemba 2019 katika Baraza la Maaskofu. Padre Aemilius anatoka katika Familia nzuri ya Montevideo, bibi yake ni myahudi lakini wazazi wake ni wasio amini na Gonzalo Aemilius aliongoka wakati  bado yuko kwenye masomo ya shule ya sekondari.

Alikuwa ni mwenye tabasamu na furaha katika uso wake kwa mapadre waliokuwa wanasaidia watoto wa barabarani licha ya vitisho vya kifo. Katika maisha yake aliamua kuwa upande wa vijana maskini na waliochwa peke katika nchi yake. Alizaliwa kunako tarehe 18 Septemba 1979, na kupewa daraaja la upadre kunako tarehe 6 Mei 2006. Padre Aemilius alikuwa tayari amekuwa amejulikana sana kwa maana siku ile asubuhi ya tarehe 17 Machi 2013 wakati Papa anasalimia waamini waliokuwa wamekusanyika nje ya Lango kuu la Mtakatifu Anna, aliweza kumwona kati ya umati wa watu na kumkaribisha amfuate katika Kanisa, mahali ambapo alikuwa anakwenda kusali misa ya kwanza na waamini mara baada ya kuchaguliwa. Baada ya liturujia ya Misa, Papa Francisko alimwita karibu naye na alikuwa amemwakilisha kwa wote ili wasali kwa ajili yake na kazi yake na vijana wa barabarani.

Padre Aemilius hata hivyo amekuwa pia Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Jubilar Juan Pablo II, yaani ya Yohane Paulo II. Katika mahojiano na Osservatore Romano, baadaye alikuwa amesimulia ni kwa jinsi gani tangu wakati huo, Papa Francisko alikuwa anamshangaza kwa uwezo wake wa kufungamanisha thamani tofauti na kuziweka katika mwelekeo mmoja. “kufanya uzoefu wa uwezo wake umekuwa ndiyo uamuzi wa maisha yangu. Amenifundisha kujitoa binafsi, suala ambalo limo ndani ya kila mmoja hata kama kila mmoja anaweza kuwa tofauti na wengine, na kuweka matunda kwa ajili ya wema wa wote.” alisema Padre Gonzalo.

Padre wa Uruguay aliyechaguliwa na Papa Francisko atakuwa karibu na Katibu wa sasa maalum Yoannis Lahzi Gaid.

26 January 2020, 15:45