Tafuta

Bwana  Georgios F. Poulides,Balozi wa Cipro, ametoa heri nyingi kwa Papa kwa niaba ya wanadiplomas na wa wawawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vatican tarehe 9 Januari 2020 Bwana Georgios F. Poulides,Balozi wa Cipro, ametoa heri nyingi kwa Papa kwa niaba ya wanadiplomas na wa wawawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vatican tarehe 9 Januari 2020 

Mabalozi wampongeza Papa kuwapa matumaini watu wengi!

Katika mkutano wa Papa Francisko na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Vatican,Bwana Georgios F.Poulides,Balozi wa Cipro,ametoa heri nyingi kwa Papa kwa niaba ya wanadiplomasia pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vatican huku akimshukuru kwa huduma yake isiyo na kifani hasa kwa ajili ya mazungumzo,amani,mshikamano,ukarimu fungamani na makutano kati ya vizazi

Angela Rwezaula - Vatican

Mwakilishi wa Wanadilomasia pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vatican Bwana   Georgios F. Poulides, ambaye ni Balozi wa Cipro, ametoa heri nyingi kwa Papa Francisko  kwa niaba ya mabalozi  hao  na kumshukuru kwa huduma yake kubwa anayoitenda katika Kanisa kwa jamii ya watu wa Mungu. Amesema  hayo wakati wa mkutano na Papa na mabalozi wote Alhamisia asubuhi, tarehe 9 Januari 2020, ambapo huu ni  utamaduni  wa kila mwaka kutakiana matashi mema wakati wa kuanza mwaka mpya. Akianza hotuba yake Bwana Poulides amesema kwa hakika ni mwaka mmoja  ambao walipata kukutana na mkutano unaofafana na ambao Papa aliwaalikwa wawe na imani katika thamani za kidiplomasia kimataifa. Kwa maana hiyo amekumbua hali halisi ambayo inaonekana dunia katika mataifa mengi yaliyojaa migogoro na mbayo anasema ni kama vita ya tatu ya dunia iliyogawanyika vipande vipande. Katika nyakati zilizopita hukosefu wa kidiplomasia ya majadiliano ilisababisha vita, joto au baridi, lakini hata leo hii bado kuna fursa ya kuweza kuzuia makosa ya wakati uliopita

Ishara na maneno ya Papa katika ziara za mwaka 2019

Mwakilishi wa  Mabalozi hao kwa maana hiyo ameweza kuwa na mtazamo mpana wa mwaka 2019 uliongazia ziara za kitume za Papa Francisko,  kwa kuanza na ile ya Nchi za  Falme za uharabuni, mahali ambapo  alioweza kutia sahihi katika Hati ya Udugu kibinadamu pamoja na Imam Mkuu wa Al Azhar, Ahmad Al-Tayyeb, na Morocco mahali ambapo alielekeza mambo muhimu ya kufuata kama jamii iliyo wazi, yenye watu wengi na mshikamano, maendeleo na kuchukua wajibu mkuu bila kuacha kuendeleza utamaduni wa majadialiano na makutano. Balozi Poulides amkumbusha pia mwaliko wa Papa kwa Wakristo wa Makanisa mbalimbali ili kujitambua kama ndugu katika utofauti, wakati wa ziara ya kitume nchini Romania, Bulgaria na Macedonia ya Kaskazini.

Asia na Afrika wito wa mshikamano na amani

Katika ziara za kitume barani Asia, Mwakilishi  wa kidiplomasia amesisitiza juu ya kazi ya Papa katika ulazima wa maadili ya ulimwenguni inayohusu mshikamano na ushirikiano.  Huu aliusisitiza nchini Thailand na makaribisho kwa wahamiaji na chini Japan kwa kutangaza juu ya uthibiti ya silaha za kinyuklia ukizingatia kwamba amani “amani haiwezi kujengwa juu ya hofu na  uharibifu wa pande zote”. Na Na kwa mtazamo wa Afrika  Mwakilishi wa Mabalozi  ameweka msisitizo wa hatua za Papa juu ya amani na upatanisho, mambo ambayo yako katika mchakato halisi wa sasa duniani kwa ujumla. Nchini Msumbiji, Madagascar na Mauritius, Papa aliwatia moyo wa kuendelea  kuimarisha amani na kuwashauri kuheshimu mazingira, haki kijamii na ufungamanishwaji kati ya kabila na tamaduni.

Elimu na majadiliano kati ya kizazi

Kadhalika Balozi Georgios F. Poulides  anataja nafasi msingi ambayo Papa anasikiliza kizazi huku akikumbuka tukio lijalo la tarehe 14 Mei liliopendekezwa na Papa Francisko kwa lengo la kuunda kwa mapana na marefu  ule mshikamano wa kielimu kati  ya sehemu zote za kijamii kwa vijana.

Upendo kwa binadamu

Hatimaye Balozi anamshukuru Papa Francisko ambaye anaendelea kusukuma mbele Kanisa na wote ili kutazama kwa upendo na matumaini ya binadamu katika karne ya XXI. Ubinadamu ambao yeye mwenyewe, unashauri ni katika kuhamasisha wito wa kutenda ndani binafsi na bila kuogopa mabadiliko”.

09 January 2020, 13:47