Tafuta

Vatican News
Kardinali Giovanni Re ni Dekano Mpya wa Baraza la Makardinali Kardinali Giovanni Re ni Dekano Mpya wa Baraza la Makardinali 

Kardinali Giovanni Re ni Dekano mpya wa Baraza la Makardinali!

Uchaguizi wa Dekano na Makamu Dekano wa Baraza la Makardinali,uliofanywa na makardinali umeridhiwa na Papa Francisko.Kwa maana hiyo wamechaguliwa Karidinali Giovanni Battista Re na Kardinali Leonardo Sandri.

Tarehe 18 Januari 2020 Papa Francisko ameridhia uchaguzi iliofanywa na Makardinali katika Baraza la Maaskofu, na Dekano wa Baraza la makardinali, ambapo wamemchagua Kardinali Giovanni Battista Re kuwa Decano, aliyekuwa na Kanisa la Suburbicaria ya Sabina-Poggio Mirteto, na sasa atakuwa na Kanisa la Suburbicaria ya Ostia.

Na wakati huo huo tarehe 24 Januari 2020, Papa Francisko ameridhia uchaguzi wa Makamu Dekano wa Baraza hilo la Makardinali kwa Jina la Kardinali Leonardo Sandri, aliye na Kanisa la Watakatifu Biagio na Carlo huko Catinari, na ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki.

26 January 2020, 10:39