Tafuta

Vatican News
Mtumishi wa Mungu Padre Luigi Sturzo aliyetambua kuunganisha maisha ya kijamii na Kanisa katika kuleta maana ya demokrasia katika jamii ya Italia Mtumishi wa Mungu Padre Luigi Sturzo aliyetambua kuunganisha maisha ya kijamii na Kanisa katika kuleta maana ya demokrasia katika jamii ya Italia  

Kard.Becciu:Padre Sturzo ni shuhuda wa Injili ya haki na tumaini!

Katika kufunga mwaka uliotolewa kwa Padre Sturzo,Kardinali Becciu katika mahubiri wakati wa Misa Takatifu iliyoadhimishwa huko Caltagirone,wilayani Catania nchini Italia amekumba sura ya Padre wa Sicilia ambaye hata leo hii anatia moyo wa kukuza zile thamani za kibinadamu na Wakristo ambao huunda urithi bora na muhimu barani Ulaya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Sura ya  kuhani na  aliyekuwa kiongozi  wa serikali, kwa jitihada zake alifanya  kuibuka kwa jumuiya na jamii halisi ya kidemokrasia. Na huyo ni Padre Luigi Sturzo, ambaye amebainishwa na Kardinali Giovanni Angelo Becciu, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza Watakatifu wakati wa hitimisho la Mwaka uliokwa  “kumbukumbu ya Padre Sturzo” aliyetangazwa kwa mwaka wa Chama cha Watu wa Italia.

Utakatifu ni kufanana na Mungu

Katika misa hiyo Jumamosi jioni majiara ya Ulaya tarehe 18 Januari 2020, Kardinali Becciu amesema, kuishi upendo wa Mungu na jirani ndiyo njia ya kufika  utakatifu na ambao unajikita katika kufuata Injili. Sura hii ya kihistoria ya ukatoliki nchini Italia, imejionesha katika jitihada za kijamii kwa wakatoliki na ambao bado wanapaswa kupyasha katika  ushiriki wa maisha hai ya ukatoliki katika nchi. Na hizi ndizo zilikuwa jitihada za mpango wa maisha ya watu kijamii, na mhuri wa kidemokrasia wa kikristo.  Alikuwa shuhuda katika Jamii hasa katika Injili ya haki na matumaini. Mtumishi wa Mungu Padre Sturzo alijikita na roho ya uadilifu, huru na nguvu katika uwanja wa kisiasa: Aliweka  yote katika kitovu cha Mungu na sababu ya maisha yake, kabla ya kila kitu! Katika sala alikuwa anachota nguvu ya kiroho na kutoa huduma kwa wema wa pamoja huku akipinga pia hata uzoefu mgumu wa kutokuelewana, kwa madai na hata kukataa uchungu amesema Kardinali Becciu.

Kukuza uraia  wa nchi

Padre Sturzo, Kardinali Becciu amemeendelea kusema,  Yeye hakuacha kuelekeza na kuheshimu mipaka sahihi kati ya siasa na dini, katika imani hiyo, Serikali  na Kanisa zinaalikwa  kushirikiana kwa ajili ya ustawi wa watu wale wale, lakini kwa utofauti ulio wazi wa nafasi za majukumu na ustadi, amebainisha Kardinali Becciu. Aidha akiendelea, kwa mujibu wa Kardinali Becciu, Padre Sturzo alikuwa mwamasishaji mzuri  na mlezi wa maono ya kikristo  katika  uraia wa serikali ambao siyo upinzani au tofauti, lakini ni heshima na ushirikiano kati ya jumuiya ya raia na ule ya kikanisa kwa ajili ya wema wa kweli wa mwanadamu na familia ya binadamu.

Ushiriki wa maisha ya kijumuiya na taa

Hata leo hii Padre Sturzo anakumbusha wakristo kwamba wanapaswa kuwajibika katika kushiriki katika  maisha ya kijumuiya, huku wakijitahidi hata katika masuala ya kisiasa ambayo  ni mtindo ulio wa juu kabisa wa upendo kama alivyokuwa amethibitisha hata Mtakatifu Paulo VI. Ni wito uliowekwa wa huduma na ambao unapatikana kwa maana ya  hisia za taasisi. Vile vile hata leo hii, anaongeza Kardinali Becciu kuwa, Padre Sturzo anaendelea kuangaza safari ya Italia na Kanisa.Ushuhuda wake wa imani na mafundisho yake  Jamii-siasa, ni urithi mkubwa kwa nchi ya Italia na ambao unazidi kuombwa ueleweke, uhifadhiwe,utafakariwe, na kushuhudiwa hata nje ya mipaka ya kitaifa.

Padre Sturzo alikuwa ni mtu wa huduma ya pamoja ambayo hata leo hii yeye anzaidi kualika na kutia moyo wa kukuza zile thamani za kibinadamu na wakristo ambao wanaunda utajiri bora na muhimu kwa urithi wa Ulaya. Yeye alitoa maisha yake kwa ustaarabu ambao katika karne nyingi umesababisha kuibuka kwa jamii za kidemokrasia za kweli. Bila misingi ya maadili, Kardinali amehitimisha  demokrasia  iko hatari ya kudhoofika kwa muda na hata kutoweka!

19 January 2020, 11:02