Tafuta

Kikundi cha wanasarakasi waliotembelea Hospitali ya watoto Bambino Gesù tarehe 17 Januari 2020 Kikundi cha wanasarakasi waliotembelea Hospitali ya watoto Bambino Gesù tarehe 17 Januari 2020 

Hospitali ya Bambino Gesù:tabasamu ni sehemu ya tiba ya magonjwa!

Siku ya sherehe imefanyika katika Hospitali ya Watoto Bambino Gesù mjini Roma kwa njia ya Kikundi cha Mchezo wa Sarakasi cha Rony Roller na ambao wametembelea watoto wagonjwa na kuwapelekea rangi na furaha kubwa.Mwenyekiti wa Hospitali hiyo,Bi Mariella Enoc amesema tabasamu ni sehemu ya tiba ya wagonjwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Michezo mingi na sarakasi, mashujaa katika mavazi na uchezaji, wasanii wa kikundi cha sarakasi cha Rony Roller na ambao walipewa tuzo katika Tamasha la Montecarlo, walifurahisha siku ya watoto waliolazwa katika Hospitali ya Bambino Gesù, Roma tarehe 17 Januari 2020. Michezo ya kwanza ya ustadi na gag ilifanyika kwenye chumba cha kucheza cha ndani na baadaye onyesho zaidi lilifanyika nje kati ya piramidi kubwa  za binadamu na nguo za kuchekesha na hatimaye walizungukia  katika vyumba vya baadhi ya vitengo vya Hospitali hiyo.

‘W’ ni kikundi cha michezo cha Hospitali, kama walivyochora watoto na mchoro huo wamemzawadia Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungani ya watu, Kardinali  Peter Turkson na Bi Mariella Enoc, Mwenyekiti wa Hospitali ya Watoto Bambino Gesù. Haya ni mabaraza mawili yaliyoandaa siku ya sherrehe ya watoto kwa njia ya kufika wanasarakasi.

Magonjwa kwa kawaida yanatabia ya kutafuta kila nja kuwatenga watoto wagonjwa na wagonjwa kwa ujumla, lakini kwa kuandaa tukio kama hili ina maana kubwa ya kuweza kushinda kile ambacho ugonjwa unapelekea hasa kwa watoto. Amethibitisha hayo Kardinali Turkson.  Naye Bi Mariella Enoc amesema tabasamu ni sehemu ya tiba ya wagonjwa. Kwa njia hiyo kufanya hivyo ni katika kuwapatia angalau furaha na vichekesho kidogo na kwa maana ya kutaka kubadili maana hali halisi ya watoto hao walivyo, na kuwafanya wafarijike kidogo kwa furaha na vichekesho.

18 January 2020, 15:55