Tafuta

Vatican News
Sisi ni ndugu na wote,waamini na wasio waamini tunaweza kujenga amani na haki ulimwenguni.Na utambulisho wetu ni Yesu! Sisi ni ndugu na wote,waamini na wasio waamini tunaweza kujenga amani na haki ulimwenguni.Na utambulisho wetu ni Yesu!  (Vatican Media)

Hakuna majadiliano bila utambulisho!

Kitovu cha shughuli ya Papa na Vatican.Tarehe 3 Januari 2020 umetangazwa ujumbe wa Papa kwa ajili ya Siku ya Wagonjwa Duniani ambayo inaadhimishwa kila tarehe 11 Februari.Pia tarehe 2 Januari alitoa ujumbe kwa njia ya video inaojikita juu ya mada ya amani katika nia za maombi ya mwezi wa pili zitolewazo na Mtandao wa Kimataifa.Ikumbukwe kuwa utambulisho wetu ni kwa njia ya Yesu!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko anawaalika Kanisa ili kusali kwa ajili ya amani.  Ndiyo nia ya maombi kwa mwezi Januari 2020 uliotolewa na Mtandao wa kimataifa wa sala ya Papa. Katika ujumbe wake kwa njia ya video Papa anazungumza kwa mara nyinge tena juu ya udugu wa kibinadamu na kushauri kupambana dhidi ya itikadi zilizomo ndani ya baadhi ya madhehebu ya kidini. Papa amesema “sisi ni ndugu na wote, waamini na wasio waamini tunaweza kujenga amani na haki ulimwenguni. Kwa Munu sisi sote ni watoto wake kama Baba anavyopenda kuunganika na siyo kugawanyika.

Majadiliano na utamaduni wa makutano kwa njia ya mapendekezo ya Papa Francisko siyo ya kubatilisha au kufuta tofauti zilizopo lakini unaweza kujadiliana tu kuanzia na utambulisho. Katika ujumbe wa Siku ya Wagonjwa duniani, Papa anaonesha wazi  utumbulisho fungamani wa kikristo kwamba: “wakati mwingine itikadi za kushoto na kulia hujaribu kuvuta Kanisa kwa upande wao kwa kushtaki thamani ya maadili fulani badala ya mengine. Lakini imani hairuhusu yenyewe kufungwa na maoni ya kisiasa, chama au falsafa. Kwa maana hiyo Papa Francisko anarudia kuweka wazi kuwa, uhai wa mtu lazima ulindwe tangu kuzaliwa hadi kufa kwake. Na inahitaji wakati huo huo iwe hata kwa sababu zote na imani katika Mungu.

Kwa hivyo Papa anawataka wafanyakazi wa afya na wahudumu wote  kutetea utu na maisha ya mtu kila wakati, bila kuangukia katika vitendo vya asili ya eutanasia na usaidizi wa kifo laini au kukandamiza maisha, hata wakati hali ya ugonjwa haitabadilika. Papa anakumbuka kwamba katika visa vingine pia inahitajika kuamua kukataa dhamiri. Wakati huo huo, tunapozungumza juu ya heshima ya maisha, hatuwezi kufikiria tu kuhusu utoaji wa mimba na eutanasia. Heshima inawahusu kila mtu na hasa kwa maskini. Papa Francisko anaomba iwepo haki ya kijamii, anaomba hupatikanaji wa huduma ya afya kwa kila mtu, bila kusahau wale wanaoishi katika umaskini. Kuheshimu maisha pia ni kupambania haki anaweka wazi suala hili muhimu.

Aidha Papa Francisko tarehe 3 Januari 2020 amesema, “Leo hii Kanisa linaadhimisha Jina Takatifu la Yesu. Kutoka kwa Yesu ndipo unazaliwa utambulisho wetu. Ukristo kwa hakika ni  “alter Christus” maana yake Kristo mmoja. Ni katika Tweet yake ambapo akumbusha waziwazi kwamba, “Wokovu ni kwa njia ya jina la Yesu. Na lazima tulishuhudie hili, Yeye ndiye Mwokozi tu. Lakini utambulisho huo siyo kufungwa, siyo kutengwanishwa  au kujitenga. Waraka wa  Dominus Iesus, yaani ”Bwana Yesu” uliosainiwa na Kardinali Joseph Ratzinger ( Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI) na kuidhinishwa msimu wa kiangazi kunako mwaka  2000 na Mtakatifu Yohane Paulo II, ulisema waziwazi kuwa “Kanisa ni muhimu kwa ajili ya  wokovu, lakini lazima kuzingatie kuwa Mungu anataka kuokoa watu wote”

Ni kile kinacho julikana kuwa ni wokovu wa kwa mapenzi yake ya ulimwengu. Kwa sababu hii, hata kwa wale wasiyo washiriki wa Kanisa, wokovu wa Kristo unapatikana kwa sababu ya neema ambayo, licha ya kuwa na uhusiano wa ajabu na Kanisa, haiwatangazii rasmi ndani yao, walakini inawaangazia  vya kutosha katika hali zao za ndani na mazingira.

Neema hii itokayo kwa Kristo ni tunda la dhabihu yake na inawasilishwa na Roho Mtakatifu.  Yesu pia yuko karibu na wale ambao hawajui. Lakini kwetu sisi ambao tunajua ni vizuri kurudia rudia kutaja Jina la Yesu wakati wa siku. Jina la Yesu ndani ya moyo linatupatia nguvu, linatufanya tuhisi kama yuko upande wetu na yuko pamoja nasi. Katika ulimwengu ambao unakwenda mbali sana na wokovu huo, Papa Francisko amesema sala hii ya moyo inatufanya tuone kuwa kweli wokovu upo katika Yesu tu.

04 January 2020, 14:01