Tafuta

Vatican News
Tunapokaribia mwaka tangu kutiwa sahini kwa Hati ya udugu wa kibinadamu wakati wa mkutano wa kidini huko Abu Dhabi,tarehe 4 Februari 2019, kitabu kipya kinachohusu mada hiyo kimetolewa Tunapokaribia mwaka tangu kutiwa sahini kwa Hati ya udugu wa kibinadamu wakati wa mkutano wa kidini huko Abu Dhabi,tarehe 4 Februari 2019, kitabu kipya kinachohusu mada hiyo kimetolewa   (Vatican Media)

Kard.Ayuso Guixot:Hati ya Udugu inatokana na jitihada za Mtaguso wa II wa Vatican!

Katika mwaka wa kwanza tangu kutiwa sahini kwa “Hati ya udugu wa kibinadamu kwa ajili ya amani duniani na kuishi kwa pamoja”,Gazeti la Civilta’ Cattolica limetangaza Kitabu Kipya ambacho ni Mfululizo wa rafudhi za kidigitali na ambacho kina utangulizi wake kuhusu mada hiyo na Kardinali Miguel Angel Ayuso Guixot Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini.

Udugu ni zana kwa ajili ya uwelewa wa kina na binafsi kwa kile ambacho kilitokea huko Abu Dhabi kunako tarehe 4 Februari 2019 kwa maana ya kusema: “Hati Juu ya Udugu wa Kibinadamu, uliotiwa sahihi na Papa akiwa na Imam Mkuu wa Al-Azhar, Al-Tayyib; na udugu kama mchakato wa dhati na mwenye nguvu dhidi ya changamoto ngumu za nyakati za sasa. Na hii siyo udugu kama utafutaji wa kawaida na wa kufariji, bali ni kama kigezo kinachofaa na kinachowezekana kuishi kwa umoja, na kwa maana hiyo ni kigezo cha dharura cha siasa.

Kitabu kimegawanyika katika sehemu tano

Gazeti la La Civiltà Cattolica ndivy katika kitabu rafudhi za kidigitali kilichohaririwa na mjesuit na kukuzwa kwa mapana na marefu karibu na maneno yatokanayo na mambo ya sasa. Kitabu hiki kimegawanyika katika sehemu 5 ambazo zinaunda kitabu hiko kikiwa na  Utangulizi wa Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, ambaye pamoja na kuongoza Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini pia ni Rais wa Tume kuu ya Hati ya Udugu Kibinadamu wa kuishi kwa amani na umoja, tume iliyoanzishwa kwa lengo la kutekeleza malengo kamili ya Hati hiyo.

Jitihada za Kanisa kwa ajili ya majadiliano ya kidini ni utumea asili

Huko Abu Dhabi ilikuwa ni kipindi muafaka katika uala la  majadiliano  ya kidini; ni katika ufunguzi wa dirisha jipya ili kutoa upeo wa kina katika safari ya majadiliano na hivyo kuendeleza kujikita ndani ya njia ya udugu, ya amani na kuishi kwa pamoja, anasisitiza Kardinali Guixot katika utuangulizi wa Kitabu hicho. Na zaidi ni katika muktadha wa maono yaliyoelekezwa na Mtakaguso II wa Vatican na baadaye kuendele kwa utangazaji wa Hati ya ‘Nostra Aetate’ na ‘Dignitatis Humanae’  na kuanzishwa kwa Siku ya kuombea amani dunia iliyofanyika huko Assisi na Siku ya tafakari, ya majadiliano na sala kwa ajili ya amani na haki duniani kama hija ya ukweli; hija ya amani kwa utashi wa ( Mtakatifu Yohane Paulo II na Papa Benedikto XVI). Vile vile katika utanguliz huo Kardinali Guixot anabainisha kwamba jitahada za Kanisa Katoliki kwa ajili ya mazungumzo ya kidini ambayo yanafungua njia za amani na udugu, ni sehemu ya utume wake wa asili na kueneza kwake ile mizizi ya tukio la mtaguso.

13 January 2020, 15:43