Tafuta

Balozi Henrique da Silveira Sardinha Pinto kutoka Brazil amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 6 Desemba 2019. Balozi Henrique da Silveira Sardinha Pinto kutoka Brazil amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 6 Desemba 2019. 

Bwana Henrique Pinto awasilisha hati za utambulisho kwa Papa!

Balozi Henrique da Silveira Sardinha Pinto wa Brazil amewasilisha hati za utambulisho kwa Papa Francisko Alizaliwa tarehe 19 Aprili 1956 Ni kiongozi ambaye amebobea kwa kiasi kikubwa katika masuala ya kidiplomasia tangu mwaka 1979 amewahi kuwa Katibu, mshauri, mratibu, mkuu wa Itifaki na waziri na mshauri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa nchini Brazil.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 6 Desemba 2019 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Henrique da Silveira Sardinha Pinto wa Brazil ambaye alizaliwa tarehe 19 Aprili 1956. Ameoa na amebahatika kupata watoto watatu. Baada ya kujiendeleza kwa masomo kunako mwaka 1980 akajipatia shahada ya Uzamivu katika Sheria na taratibu za uendeshaji wa kesi mahakamani kutoka Chuo Kikuu cha Kitaifa nchini Brazil. Ni kiongozi ambaye amebobea katika masuala ya kidiplomasia tangu mwaka 1979 amewahi kuwa Katibu, mshauri, mratibu, mkuu wa Itifaki na waziri na mshauri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa nchini Brazil.

Kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2013 Bwana Henrique da Silveira Sardinha Pinto alikuwa ni Balozi wa Brazil nchini Algeria. Kati ya Mwaka 2013-2016 alikuwa ni Balozi nchini Israeli. Mwaka 2017 akateuliwa kuwa ni Katibu mkuu msaidizi wa Jumuiya ya watu wa Mungu kutoka Brazil waliokuwa wanaishi ughaibuni. Kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2019 akateuliwa kuwa ni Rais Tume ya Maadili wa Shirikisho la Nchi za Bara la Asia na Pacific, MAE.

Papa: Brazil

 

06 December 2019, 16:57