Tafuta

Vatican News
Umakini wa Baba Mtakatifu Francisko katika Kanuni za kisheria Umakini wa Baba Mtakatifu Francisko katika Kanuni za kisheria  

Baba Mtakatifu aondoa siri ya mtu yeyote katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia!

Baba Mtakatifu Francisko ameondoa siri kwa mtu yeyote katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia.Kwa maana hii amefanya kuwa na uwezekano hupatikanaji wa ushuhuda wa kesi za kisheria kwa wachunguzi wa kiserikali.

Hizi ni Hati mbili ambazo zinaacha ishara, kwa maana Baba Mtakatifu Francisko ameondoa siri ya Kipapa katika kesi za  manyanyaso ya kijinsia na manyanyaso dhdi ya watoto wadogo zilizotendwa kwa upande wa makuhani  hata kuamua kubadili kanuni ya sheria inayohusu uhalifu kuhusu picha mbaya na uhalifu mkubwa zaidi wa kizuizini na usambazaji wa picha mbaya zinazohusisha watoto hadi umri wa miaka 18. Hati  ya kwanza ni muhimu yenye maandishi yaliyotiwa sahini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican ambapo inaeleza kuwa, Baba Mtakatifu tarehe 4 Desemba 2019 ameamua kuondoa siri ya mashtaka, ya michakato na maamuzi  kuhusu uhalifu uliotajwa katika makala ya kwanza na motu proprio ya hivi karibuni iitwayo “Vos estis lux mundi”.

Hiyo ina maana ya kusema ni katika kesi za dhuluma na vitendo vya kijinsia vinavyofanywa chini ya vitisho au udhalilishaji wa mamlaka; kesi za unyanyasaji wa watoto na watu walio katika mazingira magumu; kesi za picha mbaya za watoto; kesi za kutoripoti na kuwafunika wanyanyasaji kwa upande wa maaskofu na wakuu wa mashirika ya dini. Maagizo mapya yanataja kuwa, taarifa zinatolewa kwa namna ya kuhakikisha usalama wake, uadilifu na usiri uliowekwa na Kanuni ya Sheria ili kulinda sifa nzuri, picha na nyanja ya kibinafsi  ya watu wanaohusika. Lakini siri ya ofisi  haizuizi kuwa na utimilifu wa majukumu yaliyowekwa katika kila mahali kwa mujibu wa sheria za undeshaji wa serikali, pamoja na majukumu yoyote ya kuripoti na utekelezaji wa maombi ya utendaji wa mamlaka za mahakama za serikali. Na zaidi kwa wale wanaotoa ripoti hiyo, kwa wale ambao ni waathirika na kwa mashuhuda, hakuna kizuizi cha kuwa na ukimya juu ya matendo hayo.

Na maelekezo ya pili yaliyotiwa sahini na Katibu  huyo huyo wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin na Rais wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa Kardinali Luis Ladaria Ferrer, zimetangaza hata kuhusu mabadiliko katika makala  tatu za motu Proprio ya “Sacramentorum sanctitatis tutela” (ya 2001, ambayo tayari ilifanyiwa mabadiliko kunako mwaka 2010). Katika uthibitisho huo inasema kuwa "upatikanaji au kuhamisha au kuenezwa, kwa lengo la tamaa za mwili, za picha mbaya za watoto wadogo wenye umri wa miaka 18 kwa upande wa makuhani, kwa namna yoyote na kwa chombo chochote” ambapo hadi leo ilikuwa imewekwa kikomo cha miaka 14, kwamba ni uhalifu mkubwa kabisa unaostahili  hukumu kutoka Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa.

Na katika kifungu kingine, hatimaye inaruhusiwa kwamba, katika kesi zinazo husiana na uhalifu huu mbaya zaidi, wanaweza kutumia nafasi yao mawakili na waendesha mashtaka hata waamini walei ambao wametunikiwa shahada ya udaktari wa Kanuni ya Sheria iliyoidhinishwa na Rais wa Chuo ili kuweza kuchukua jukumu na siyo mapadre tu peke yake.

17 December 2019, 12:30