Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Rais Nicos Anastasiades wa Cyprus: Muungano wa Visiwa, Wakimbizi, Wahamiaji; Uhuru wa Kuabudu. Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Rais Nicos Anastasiades wa Cyprus: Muungano wa Visiwa, Wakimbizi, Wahamiaji; Uhuru wa Kuabudu.  (Vatican Media)

Rais Nicos Anastasiades wa Cyprus akutana na Papa Francisko!

Baba Mtakatifu Francisko na Rais Nicos Anastasiasiades wa Cyprus wamejadili masuala tete yanayopewa kipaumbele cha pekee katika maisha yao, yaani: ukarimu kwa wakimbizi na wahamiaji na changamoto zake; uhuru wa kuabudu na uhuru wa kidini; pamoja na haki msingi za makundi madogo madogo katika jamii. Wamehimiza umuhimu wa kujenga na kudumisha amani duniani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 18 Novemba 2019 amekutana na kuzungumza na Rais Nicos Anastasiades wa Cyprus, ambaye baadaye, amekutana pia na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili wamegusia uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili na kujikita zaidi katika mchakato unaopania kuviunganisha Visiwa viwili.

Baba Mtakatifu Francisko na mgeni wake, wamejadili pia masuala tete yanayopewa kipaumbele cha pekee katika maisha yao, yaani: ukarimu kwa wakimbizi na wahamiaji na changamoto zake; uhuru wa kuabudu na uhuru wa kidini; pamoja na haki msingi za makundi madogo madogo katika jamii. Mwishoni mwa mazungumzo yao, Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Rais Nicos Anastasiades wa Cyprus wamepembua hali ilivyo huko Mashariki wa Bahari ya Mediterrania na kuhimiza uhimu wa kusimama kidete ili kujenga na kudumisha amani na utulivu kwa njia ya majadiliano; kwa kuheshimu haki msingi za binadamu na itifaki na sheria za kimataifa.

Papa: Rais wa Cyprus
18 November 2019, 14:28