Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu amemteua Dr. Carmelo Barbagallo kuwa Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF. Baba Mtakatifu amemteua Dr. Carmelo Barbagallo kuwa Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF. 

Dr. Carmelo Barbagallo, Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za kifedha, AIF.

Dr. Carmelo Barbagallo ameteuliwa kuwa Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF. Ni kiongozi aliyebobea kwenye masuala na shughuli za kibenki. Amekuwa ni mshauri mkuu wa Benki Kuu ya Italia kuhusu usimamizi wa Benki, Masuala ya Fedha yaani “Single Supervisory Mechanism (SSM). Huu ni mfumo unaosimamia na kuratibu Benki mbali mbali Barani Ulaya.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Dr. Carmelo Barbagallo kuwa Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF. Ni kiongozi aliyebobea kwenye masuala na shughuli za kibenki. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni mshauri mkuu wa Benki Kuu ya Italia kuhusu usimamizi wa Benki, Masuala ya Fedha kama yanavyojulikana kitaalamu “Single Supervisory Mechanism (SSM). Huu ni mfumo unaosimamia na kuratibu Benki mbali mbali Barani Ulaya. Dr. Carmelo Barbagallo alizaliwa tarehe 28 Februari 1956 huko Catania, Italia. Amefunga ndoa na kubahatika kupata watoto wawili. Baada ya masomo na majiundo yake katika masuala ya kifedha, kunako mwaka 1980 alijiunga na Benki Kuu ya Italia, akajihusisha sana na masuala ya tafiti za kiuchumi, usimamizi wa shughuli za kifedha kimataifa na vitega uchumi. Kwa upande wake, Dr. Carmelo Barbagallo anapenda kumshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kumteua kuwa Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF na kwamba, uteuzi huu anakumbatia uzito wa kimaadili na kitaalam.

Hii ni changamoto ya kuhakikisha kwamba, anatumia kikamilifu karama, uzoefu na mang’amuzi na weledi aliojichotea kutoka Benki Kuu ya Italia, kwa ajili ya kuendeleza huduma ya Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican. Anasema ataendelea kuhakikisha kwamba, kunakuwepo na ukweli na uwazi katika masuala ya habari za kifedha; kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Hii ni changamoto pia ya kuendelea kushirikiana na kushirikamana na taasisi mbali mbali za kifedha duniani, ili hatimaye, kufikia malengo yaliyobainishwa na Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF. Wakati huo huo, Uongozi wa Benki Kuu ya Italia unapenda kuchukua fursa hii kumpongeza Dr. Carmelo Barbagallo kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF, hali itakaoendelea kuimarisha uhusiano kati ya Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican pamoja na Benki Kuu ya Italia.

Papa: Uteuzi

 

28 November 2019, 16:47