Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Imam Mkuu Ahmed Al-Tayeb mjini Vatican tarehe 15 Novemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Imam Mkuu Ahmed Al-Tayeb mjini Vatican tarehe 15 Novemba 2019  (ANSA)

Baba Mtakatifu amekutana na Imam Mkuu Ahmed Al-Tayeb

Tarehe 15 Novemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Imam Mkuu Imam Ahmed Al-Tayeb wa Al-Azhar.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Asubuhi ya tarehe 15 Novemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Imam Mkuu Ahmed Al-Tayeb, Sheikh wa Al-Azhar, akiwa amesindikizwa na Waziri Mkuu wa Nchi za Falme za Uarabuni, Bwana Saif bin Zayed Al Nahyan, Balozi wa Jamhuri ya nchi ya Misri aliyewakilisha mjini Vatican Bwana Mahmoud Samy na baadhi ya watu wakuu  wengine na wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar pamoja na Tume Kuu kwa ajili ya mchakato wa kufikia malengo yaliyomo kwenye Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa ajili ya amani duniani na kuishi kwa pamoja iliyoundwa mwezi Agosti mwaka huu. Pamoja nao, pia walikuwapo wawakilishi wa Vatican Kardinali Miguel Angel Ayuso Guixot, Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na Monsinyo Yoannis Lahzi Gaid, Katibu muhtasi wa Baba Mtakatifu.

Mada ya ulinzi wa watoto katika dunia ya kidijitali

Katika mazungumzo yao wamegusia  juu ya mada ya ulinzi wa watoto wadogo duniani katika dunia ya kidijitali ambayo ndiyo mada katika wiki hii inazungumza, pia kukumbuka hata ziara ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoifanya katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu. Kadhalika viongzoi hawa pia wamezungumzia suala la kuanzishwa kwa  Tume Kuu kwa ajili ya kufikia malengo ya Hati ya Udugu wa Kibinadamu iliyoundwa mwezi Agosti mwaka huu, ambapo wajumbe wa Tume hiyo wamemwakilisha mjube mwingine mpya Dk. Irina Georgieva Bokova, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa UNESCO (2009-2017) na kumwonyesha Baba Mtakatifu juu ya Mpango uitwao “ Nyumba ya Ibrahimu”uliozinduliwa huko New York, Marekani mwezi Septemba mwaka huu.

15 November 2019, 11:08