Tafuta

Askofu mkuu Ernest Ngboko Ngombe, Jimbo kuu la Mbandaka-Bikoro, DRC. Askofu mkuu Ernest Ngboko Ngombe, Jimbo kuu la Mbandaka-Bikoro, DRC. 

Askofu mkuu mteule Ernest Ngboko Ngombe, Jimbo kuu la Mbandaka-Bikoro, DRC.

Askofu mkuu mteule Ernest Ngboko Ngombe alizaliwa tarehe 25 Mei 1964 Jimboni Lisala. Akaweka nadhiri zake za kwanza, Oktoba 1987 na Upadrisho tarehe 20 Juni 1996 huko Dakar, Senegal. Kunako mwaka 2011 aliteuliwa kuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Kitaalimungu iliyoko nchini Cameroon na Mratibu wa Shirika, Kanda ya Afrika. Mwaka 2015 akateuliwa kuwa Askofu wa Lisala.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Ernest Ngboko Ngombe, C.I.C.M, kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mbandaka-Bikoro, nchini DRC. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Ernest Ngboko Ngombe alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lisala nchini DRC. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Ernest Ngboko Ngombe alizaliwa tarehe 25 Mei 1964 Jimboni Lisala.  Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa nchini Cameroon, aliweka nadhiri zake za kwanza hapo tarehe 17 Oktoba 1987 na baadaye kupadrishwa tarehe 20 Juni 1996 huko Dakar, Senegal.

Tangu wakati huo katika maisha na utume wake kama Padre amekuwa Paroko msaidizi, Mkuu wa Shirika mahalia na kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2011 alipelekwa kujiendeleza kwa masomo ya juu katika masuala ya kitaalimungu na kujipatia Shahada ya Uzamili kutoka katika Chuo Kikuu cha “Catholic Theological Union”, kilichoko nchini Marekani. Kunako mwaka 2011 aliteuliwa kuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Kitaalimungu iliyoko nchini Cameroon na Mratibu wa Shirika, Kanda ya Afrika. Kunako mwaka 2011 hadi mwaka 2015 alikuwa ni Makamu mkuu wa Shirika na makazi yake yakiwa mjini Roma. Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 11 Februari 2015 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lisala, nchini DRC.

Jimbo Katoliki DRC
26 November 2019, 15:00