Tafuta

Vatican News
Dk. Gisotti amebainisha kuwa ni muhimu mawasiliano ya Kikristo yasiwe ya ushindani kwa sababu sisi tunao mtindo ambao hauna kiburi wala nguvu. Dk. Gisotti amebainisha kuwa ni muhimu mawasiliano ya Kikristo yasiwe ya ushindani kwa sababu sisi tunao mtindo ambao hauna kiburi wala nguvu.  (Vatican Media)

Dk.Gisotti:wanahabari katoliki wawe sauti na masikio ya Papa na Kanisa!

Baba Mtakatitu Francisko mara nyingi anatutaka wanahabari turudishe utaratibu wa kutoa habari huku tukitoa sauti kwa niaba ya wale wasio na sauti. Kama Kanisa linalotaka kutoka nje ili kuweza kutoa habari kwa wale walio wa mwisho na ambao wamepotea,kwa wa maana hiyo mwandishi wa habari na hasa katoliki lazima awe karibu na watu na kila mtu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Dk. Alessandro Gisotti, mkurugenzi msaidizi wa Uwariri wa Baraza la kipapa la Mawasialino Vatican ambaye hivi karibuni alikuwa ndiye Msemaji wa mpito wa vyombo vya Habari Vatican, wakati akitoa hotuba yake kwa wanahabari wa kanda mawasiliano kijamii waliounganika katika makao makuu ya Baraza la Maaskofu Italia  (CEI) kwenye mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Baraza la Maaskofu kitaifa, Italia, ameangazia juu ya utume wa mawasiliano hasa katika kutoa sauti kwa niaba ya wasio kuwa na sauti.

Dk. Gisotti katika hotuba yake amesema, inabidi kufanya mitandao na kushirikiana kwa kufanya juhudi za mawasiliano ili ziweze kuwa na ufanisi zaidi katika kuongeza rasilimali iliyowekezwa. Ni muhimu kuwa mwangalifu wa kutosongwa ndani ya bahari ya fursa, kwa sababu hata ikiwa teknolojia iko mikononi, haimaanishi kwamba barabara zote lazima zitifuliwe na ndiyo maana kuna ulazima wa kufanya mang’amuzi katika uchaguzi na sio tathmini tu ya gharama na faida.

Ni lazima tuwe sio sauti ya Papa na Kanisa tu, bali pia  kuwa kama masikio yao na ili kuweza kusikiliza watu wanafikiria nini na wanahisi nini, anamesisitiza Dk. Gisotti na wakati huo huo amebainisha kuhusiana na mbio za habari. “Kasi za mawasiliano za kupita kiasi zimebadilisha jinsi tunavyo wasiliana” anasema, huku akitoa mfano kwamba  “ikiwa msemaji wa ofisi ya waandishi hapo awali alikuwa na masaa 24 ya kujibu swali kutoka kwa waandishi wa habari, kwa sasa ana dakika 24 tu”. “Lakini tunahitaji kufikiria juu ya mawasiliano, ni muhimu kuwa na wakati wa kuyafanya”. Kwa Mujibu wa Dk. Gisotti anasema “ni muhimu kwamba Mawasiliano ya Kikristo hayapaswi kuonekana  ya ushindani, kwa sababu sisi tunao mtindo ambao hauna kiburi wala kutumia nguvu”.

Akiendelea na msisitizo wa jinsi gani ya kutoa habari amesema, lugha na mtindo ambao tunatumia, kwa hakika,unazidi kuchukua hatua katika njia yetu ya kuwasiliana na kwa maana hiyo, "tuna jukumu la kutunza lugha na maneno. Mara nyingi hata kati ya Wakristo, hasa kwenye mitandao ya kijamii  hushikana wao kwa wao kwa kutumia hata lugha za vivumishi”. Lakini sisi ni mashuhuda wa kila siku wa habari ambazo zimekuwa zikiendelea kwa miaka elfu mbili. Na habari hii ina nguvu ya kipekee ya kuleta mabadiliko, kama inavyo shuhudiwa na Baba Mtakatifu Francisko. Aidha kwa kuongeza amesema, mara nyingi Baba Mtakatifu anatutaka turudishe utaratibu wa kutoa habari huku tukitoa sauti kwa niaba ya wale wasio na sauti. Kama Kanisa linalo taka kutoka nje ili kuweza kutoa habari kwa wale walio wa mwisho na kwa wale ambao wamepotea na kwa wa maana hiyo mwandishi wa habari, hasa katoliki lazima awe karibu na watu na kila mtu.

01 October 2019, 15:04