Tafuta

Vatican News
Ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya video kwa nia ya maombi ya mwezi Oktoba 2019 ni kusali kwa ajili ya uamsho wa dhamiri ya kimisionari Ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya video kwa nia ya maombi ya mwezi Oktoba 2019 ni kusali kwa ajili ya uamsho wa dhamiri ya kimisionari  (Vatican Media)

Ujumbe wa Papa kwa njia ya video wa nia ya maombi kwa mwezi Oktoba 2019

Katika nia za maombi ya mwezi Oktoba 2019, Baba Mtakatifu Francisko anawalenga wakatoliki wote waweze kukabiliana na changamoto ya kutangaza Yesu aliyekufa na kufufuka

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa njia ya sala, wakatoliki wote waweze kukabiliana na changamoto muhimu zaidi hasa za kuwa na mwamko mpya wa shughuli za umisionari wa Kanisa. Na ndiyo mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko anao utoa kwa njia ya video kwa mwezi Oktoba 2019 ulioandaliwa na Mtandao wa Utume wa Sala Kimataifa ili kueneza kila mwezi nia zake za maombi.

Maadhimisho ya miaka 100 ya Wosia wa Maximum illud

Nia za Baba Mtakatifu kwa mwezi Okotba inaongozwa na mada ya maadhimisho ya miaka 100 ya Wosia wa Kitume wa Maximum Illud wa Papa Benedikto XVI kunako mwaka 1919. Kwa maana hiyo ipo sababu kubwa ya kuhamasisha ari ya kimisionari na uamsho wa dhamiri kama kielelezo cha miaka hii ya utume wake ambao umejifafanua katika Wosia wa Kitume wa Evangelii gaudium wa Baba Mtakatifu  Francisko alipotangaza Mwezi Maalum wa Kimisionari Oktoba 2019 kwa kuongozwa na  kauli mbiu Mmebatishwa na kutumwa; Kanisa ka Kristo katika utume ulimwenguni. Matendo ya umisionari  ni sawa sawa na matendo ya kila shughuli ya Kanisa anasisitiza Baba Mtakatifu Franxcisko katika ujumbe wake kwa njia ya video.

Mwaliko wa Baba Mtakatifu katika ujumbe wa video

Leo hii kuna ulazima wa mwamko mpya wa shughuli za kimisionari katika Kanisa ili kukabiliana na changamoto ya kutangaza Yesu aliyekufa na kufufuka. Na hii inahitaji kufikia pembezoni, katika maeneo ya kibinadamu, maeneo ya kiutamaduni na  kidini, ambayo ni mageni kuhusu Injili. Hiyo ndiyo maana ya kile kinaoitwa Missio gentes yaani utume wa watu anathibtisha! Kukuza na kuwa na moyo wa utume wa Kanisa ni sala. Katika Mwezi Maalum wa kimisonari, Baba Mtakatifu Francisko anasema, tusali ili Roho Mtakatifu awezeshe uchupukizi mpya wa umisionari kwa ajili ya wabatizwa wote na waliotumwa na Kanisa la Kristo.

Jinsi gani ya kuishi siku 31 za Mwezi Oktoba?

Ili kuishi kwa kina safari ya kila siku katika Mwezi Maalumu wa Kimisionari kuna kitabu ambacho ni kiongozi kinapatika katika duka la vitabu Pauline, chenye jina “ mmebatiwa na kutumwa:Kanisa la Kristo katika utume duniani .  Aidha Chama cha Kitume cha Vijana wa Ekaristi ambao ni Mtandao wa Utume wa Sala pamoja na mambo mengine unajihusisha kikamilifu katika kuandaa picha za video zinazosindikiza nia za Baba Mtakatifu kwa kila mwezi (www.ilvideodelpapa.org) pamoja na Jukwaa la Sala kwa ajili ya utume wa Kanisa (www.clicktopray.org).

02 October 2019, 12:32