Tafuta

Taarifa ya Sinodi ya Amazonia kwa waandishi wa habari:hakuna haki ya mwanadamu yoyote kuondolewa kwa nguvu katika ardhi yake asilia Taarifa ya Sinodi ya Amazonia kwa waandishi wa habari:hakuna haki ya mwanadamu yoyote kuondolewa kwa nguvu katika ardhi yake asilia  

Sinodi ya Maaskofu:Injili ni tangazo la maisha mapya kwa wote!

Hali za watu asilia,uinjilishaji na utamadunisho ndiyo mtazamo wa mada zilizotolewa tarehe 17 Oktoba 2019 kwa waandishi wa habari.Mashuhuda kutoka Brazil,Askofu Mkuu Paloschi,Padre Justino S.Rezende,Dk.Felicio de Araujo Pontes Junior;Sauti ya wanawake ni kiongozi wa watu asilia kutoka Ecuador Patricia Gualinga na Guyana ni Leah Rose Casimero.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mashuhuda watatu kutoka nchini Brazil, Askofu Mkuu Roque Paloschi, Padre Justino Sarmento Rezende msalesiani, mwendesha mashtaka wa Jamhuri Dk. Felicio de Araujo Pontes Junior. Na kwa upande wa wanawake: kiongozi wa watu wa asilia kutoka Ecuador Patricia Gualinga, kutoka Guyana Leah Rose Casimero, Mratibu wa Elimu Bora ya Lugha katika Mpango wa watoto wa Wapichan. Ndizo sauti za wawakilishi kutoka Amazonia waliokuwa mstari wa mbele kuelezea masuala ya Sinodi, kwa waandishi wa habari na ambapo kwa siku mbili  Sinodi imeendelea kwenye vikao vya makundi madogo madogo huku wakipanua mawazo kuhusu mijadala iliyotolewa katika Sinodi inayoendelea Vatican. Haya yote yameelezwa na Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paulo Ruffini, tarehe 17 Oktoba 2019 mchana.

AkianzaDk. Ruffini amesema, Leah Rose Casimero, anayetoka Guyana mwenye asili ya watu asilia wa Wapichan amesimuliza uzoefu wake kama mratibu wa mpango unaotazamia mafunzo ya lugha mbili kwa watu asilia yaani lugha ya kiasili na ya kingereza. Hawa wanazo zana kwa ajili ya watoto wao na kuongezea hata zana za kiasili katika maisha yao ya kiutamaduni. Nia yao ni kutaka kuwasaidia  watu wa Asilia kwa maana hiyo Wapichan kwa njia ya mpango huo ulionzishwa kutokana na mazungumoza na Shirika la Wajesuit na makanisa mengine pia kwa msaada wa mamlaka. Aidha kwa watu asilia  hata Bi Patricia Gualinga, kiongozi wa kutetea haki za binadamu katika jumuiya iitwayo Kichwa ya  Sarayaku, nchini Ecuador.  Kwa upande wake ametoa wito kwa ajili ajili ya ulinzi wa Amazonia ambayo inatishiwa na matokeo mabaya ya ubinadamu wote. Ni wito hata wa kuwa na mshikimano na  watu asilia na Kanisa ambao wanateswa na hata kuwawa. Kadhalika katika Briefing hiyo, umakini kuhusu haki za watu wa Amazonia, hata watu wenye asili ya kiafrika, umetolewa na Bwana Felicio de Araujo Pontes Junior.  Yeye anatoka nchini Brazil na ni mwendesha mashtaka katika mahakama ya  Jamhuri ya nchi hiyo na mtaalam katika sheria za watu asilia. Mara nyingi watu hawa anasema wanapingana na mtindo unaoendelea wa maendeleo,kuzingatia umakini  juu ya kuongezeka mtindo wa kutaka kufuga utamaduni mmoja aidha  amebainisha jinsi gani wanadamu hawana haki ya kuondolewa katika mazingira kwa vigezo vya kupeperusha bendera ya maendeleo.

Aidha ushuhuda mwingine umetolewa na Padre msalesiani, Justino Sarmento Rezende, ambaye ni mtaalam wa tasaufi ya watu asilia na uchungaji wa utamadunisho. Anatoka katika watu wa asilia waitwao tuyuca nchini Brazil. Akeielezea kuhusu wito wake amesema unatokana na wamisionari waliokuwa wanafundisha katekisimu  babu zake. Aidha wito wake pia unatokana na kuwa na  shauku ya kutaka kuonyesha imani  ya lugha mama ya kuzaliwa. Amethibitisha kuwa hii imewezakana tangu Kanisa Mama  lilipotambua kuwa watu asilia kwa kuinjilishwa wangeweza kuwa pia nao wainjilishaji. Yeye ni kuhani sasa kwa miaka 25 na katika mazungumzo yake ameshukuru sana wamisionari ambao waliweza kupeleka Injili, wakiwa pia na shauku ya kutaka kuelewa utamaduni wa watu asilia. Na hiyo ndiyo iwe shughuli kuu ya kupeleka mbele kwa vumilivu na majadiliano kuhusu utambuzi wa maisha ya watu hao asilia.

Hatimaye Askofu Mkuu Roque Paloschi, wa Jimbo Kuu Katoliki Porto Velho nchini Brazili na Rais wa Baraza la Kimisionari la watu Asilia(CIMI), ameweka bayana  kuhusu haki za watu asilia ambazo zinakandamizwa na kuhusu matatizo ya ardhi ya kiutamaduni. Katiba ya mwaka 1988, amefafanua, ilikuwa inatazamia  kwamba hadi kufikia mwaka 1993 nchi zote za watu wa asilia zilikuwa ziwe zimetengwa na kupimwa, na wakati hata theluthi moja haikutengwa na zile ambazo hazikuainishwa zilivamiwa, zikiwalenga watafuta dhahabu, wenye viwanda vya madini, wenye  viwanda vya mafuta na vile vyenye  unyonyaji wa mbao. Katika maelezo yake pia amesisitiza hasa, kwamba shughuli ya uchungaji wa utamadunisho haufanyiki kama vile ni propaganda na badala yake ni ushuhuda. Hiyo siyo hali ya kulazimisha utamaduni ulio wa  juu na kufuta utamaduni wa watu wengine, badala yake ni  kuhifadhi mbegu zilizoko katika  kila utamaduni kwa sababu hakuna utamaduni ni kamili; na zaidi kutangaza Injili kiukweli ni tangazo la maisha mapya na sote tunahitaji kuwa watu wapya katika kukutana na Kristo, amesisitiza Askofu mkuu Paloshi.

 

18 October 2019, 11:21