Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteua Monsinyo Luigi Roberto Cona kuwa Mratibu mkuu wa shughuli za kiutawala mjini Vatican. Papa Francisko amemteua Monsinyo Luigi Roberto Cona kuwa Mratibu mkuu wa shughuli za kiutawala mjini Vatican.  (ANSA)

Mons. Luigi Roberto Cona ateuliwa kuratibu shughuli za utawala

Monsinyo Luigi Roberto Cona alizaliwa mwaka 1965, Italia. Alipewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 28 Aprili 1990 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Piazza Armeria. Alijiendeleza zaidi katika masomo na hatimaye, kubahatika kupata shahada ya uzamivu katika taalimungu mafundisho sadikifu ya Kanisa. Tarehe 1 Julai 2003 akaanza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Kanisa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Luigi Roberto CONA kuwa Mratibu mkuu wa shughuli za kiutawala mjini Vatican. Monsinyo Luigi Roberto Cona alizaliwa tarehe 10 Novemba 1965 huko Niscemi, Caltanissetta, Kusini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 28 Aprili 1990 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Piazza Armeria. Alijiendeleza zaidi katika masomo na hatimaye, kubahatika kupata shahada ya uzamivu katika taalimungu mafundisho sadikifu ya Kanisa. Tarehe 1 Julai 2003 akaanza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Kanisa. Tangu wakati huo, ametekeleza dhamana hii nchini Panama, Ureno, Cameroon, Uturuki na hatimaye, mwishoni, kabla ya uteuzi huu, alikuwa amepangiwa kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican katika kitengo kinacho ratibu shughuli za kiutawala mjini Vatican.

Monsinyo Cona
25 October 2019, 14:54