Tafuta

Vatican News
Kuanzia tarehe 29 hadi 31 Oktoba 2019 itafanyika semina kwa ajili ya wasimamizi wa vikanisa vya kijeshi kwa kuongozwa na mada ya haki za kibinadamu kimataifa Kuanzia tarehe 29 hadi 31 Oktoba 2019 itafanyika semina kwa ajili ya wasimamizi wa vikanisa vya kijeshi kwa kuongozwa na mada ya haki za kibinadamu kimataifa 

Kozi kuhusu haki kibinadamu kwa wasimamizi wa vikanisa vya kijeshi!

Kuanzia tarehe 29 hadi 31 Oktoba 2019 itafanyika kozi kwa ajili ya wasimamizi wa vikanisa vya kijeshi kwa kuongozwa na mada ya haki za kibinadamu kimataifa. Kozi hiyo inatarajiwa kufanyika katika Taasisi ya Baba wa Kanisa ya Agostinianum mjini Roma, ambapo washiriki ni kutoka mataifa 47 duniani. Ni katika kuchunguza na kutafakari kwa kina utume wa wasimamizi wa makanisa ya kijeshi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuchunguza na kutafakari kwa kina utume wa wasimamizi wa makanisa ya kijeshi katika kuwalinda watu wasio na uhuru, kwa kuzingatia changamoto za sasa za sheria za kibinadamu kimataifa, katika muktadha wa migogoro ya silaha, katika hali ya udhabiti mkubwa wa kibinafsi na katika visa vya udhalilishaji unaofanywa na wadau wasio wa serikali. Ndiyo  lengo la semina ya 5 ya mafunzo  kwa mapadre wasimamizi wa makanisa ya wanajeshi katoliki kwa ajili ya haki za kibinadamu kimataifa ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Maaskofu na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu kuanzia tarehe 29 hadi 31 Oktoba 2019 mjini Roma  katika Taasisi ya Masomo ya Baba na Mwalimu  wa Kanisa Mtakatifu Agostino.  Mafunzo haya ni moja ya shughuli za Makao makuu Vatican ambayo iemeendelea kujikita katika kutimiza kwenye mwelekeo wa mantiki ya   Baraza la 32 la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Nusu Mwezi mwekundu kunako mwaka 2015 kwa mujibu wa waandaaji wa tukio hili.

Ratiba ya kozi hiyo

Kwa mujibu wa waandaaji, ratiba ya tarehe 29 na 31 Oktoba inaonesha kwamba,  baada ya salam za ufunguzi wa Kozi hiyo  kutoka kwa Kardinali Marc Ouellet, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu, Kardinali Peter K.A. Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la maendeleo fungamani ya watu na  Kardinali Fernando Filoni, Rais wa Baraza la Kipapa la Unjilishi wa  watu, vile vile watafuatia hata watoa hotuba wengine, kama ifuatavyo: Wawakilishi kutoka Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa vikosi vya kijeshi na mashirika ya kimataifa, maafisa wa jeshi kutoka sehemu mbali mbali za ulimwengu, maprofesa wa vyuo vikuu.

Hata hivyo washiriki wa Kozi hii wanatoka katika Mataifa 47 tofauti duniani na ambao watakuwa ni karibia 130 na ambao tarehe 31 Oktoba wanatarajia kukutana na Baba Mtakatifu katika ukumbi wa Kitume. Siku hiyo hiyo mchana chini ya usimamizi wa Kardinali Turkson na Monsinyo Bruno Marie Duffé, Katibu wa Baraza hili watafanya meza ya mduara, katika kuenzi “maadhimisho ya miaka 70 ya Mkataba wa Geneva kunako tarehe 12 Agosti 1949” na mahali ambapo watashiriki mabalozi  waliotambuliwa na Vatican: Denis Knobel, Balozi wa Uswiss anayewakilisha nchi yake mjini Vatican; Aloysius John, Katibu  Mkuu wa Caritas Internationalis; Didier Pfirter, Kamishna wa Mkutano wa 33 wa Kimataifa wa Msalaba Mwekundu Nusu Mwezi  Mwekundu (Croce Rossa e Mezzaluna Rossa).

Maadhimisho ya misa takatifu kwa washiriki wa semina

Kufuatia na tukio hili la semina yao, ratiba ya maadhimisho ya misa takatifu imepangwa kama ifuatavyo: Kardinali Ouellet, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu, Jumanne tarehe  29 Oktoba saa 12.30 majira ya Ulaya katika Kanisa la Mtakatifu Caterina wa Siena, Magnanapoli;  Jumatano tarehe 30 Oktoba 2019 saa 1.45 majira ya Ulaya, Askofu Mkuu Santo Marcianò, wa Jimbo la Kijeshi nchini Italia ataongoza Misa takatifu katika Kanisa la Roho Mtakatifu,Sassia; hatimaye Alhamisi  tarehe 31 Oktoba 2019 saa 1.45 majaira ya Ulaya,  Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ataongoza Misa Takatifu  katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Hata hivyo pia inatarajiwa kufanyika maadhimisho ya masifu ya jioni katika kikanisa cha Kipapa kwenye Chuo cha Kipapa cha Urbaniano , Jumatano tarehe 30 Okotba 2019 saa 12.45 majiara ya Ulaya.

28 October 2019, 14:30